Popular posts from this blog
Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …
Kocha wa mpya wa muda wa klabu ya Chelsea Guus Hiddink ambaye amejiunga kwa mara ya pili kuifundisha klabu hiyo, baada ya miaka sita toka aondoke mwishoni mwa mwaka 2009 kama kocha wa muda wa klabu hiyo, Guus Hiddink ambaye ndio ameichukua Chelsea mikononi mwa Jose Mourinho ili aiokoe isiporomoke zaidi, ameanza kwa kuwatuliza mashabiki wa Chelsea kuwa wasitegemee mabadiliko ya haraka. Kwa miaka ya hivi karibuni Chelsea imekuwa ikifanya vizuri, hata msimu uliopita walikuwa Mabingwa wa Ligi Kuu Uingereza hivyo mashabiki wake wanaweza wakatarajia mabadiliko ya haraka na kutegemea kuiona timu yao ikirudi nafasi za juu, Guus Hiddinkambaye anaamini kuwa atafanya vizuri na kuirudisha Chelsea katika nafasi nzuri amewaambia mashabiki wasitegemee kuona timu inabadilika haraka kwani inahitaji muda. “Kama utaangalia msimu uliopita Chelsea walikuwa na mafanikio makubwa na kutwaa Kombe, najua msimu huu wana malengo kama hayo, kutwaa Ubingwa tena hususani katika Ligi Kuu Uingereza...
Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini
Wanafunzi wa shule za msing i mkoani Geita wamewalalamikia walimu wao kufanya kazi migodini na kuendesha bodaboda, hali inayosababisha wafeli kutokana na kutofundishwa darasani. Hata hivyo, Ofisa Elimu, Mkoa wa Geita, Eufransia Buchuma alisema juzi kuwa walimu hukimbia vipindi hali inayodhorotesha ufaulu. “Tumeweka mikakati kwa kila walimu wakuu wote kutoa taarifa kuhusu watakaoshindwa kuhudhuria vipindi au kuwa watoro, kisha hatua za kinidhamu zitachukuliwa kwa mujibu wa taratibu za kazi,” alisema Buchuma. Wakizungumza hivi karibuni, baadhi ya wanafunzi walisema hawamalizi silabasi kutokana na walimu kutokuwapo kwani siku nyingine wanarudi nyumbani bila kusoma. “Walimu hawafundishi, mnaweza kukaa wiki nzima bila mwalimu kuingia darasani, siku nyingine zote haumuoni au anakuja kusaini kisha anaondoka,” alisema mwanafunzi Retias Devid. Alisema walimu wengine wanafanya shughuli zao migodini, hivyo mwitikio wa kufundisha unakua mdogo. “Hata wakifundisha ha...