MKOA WA ILALA WAONGOZA KWA UBAKAJI, HIZI NI TAKWIMU KUTOKA TAMWA

Kaimu Katibu Mkurugenzi wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Gladnes Munuo akifafanua mbele ya waandishi wa habari wakati wa mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa TAMWA makao makuu Sinza Mori Jijini Dar es Salaam.
KILA siku wastani wa watoto watano wananajisiwa na kurawitiwa katika Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam.
           Kaimu Katibu Mkurugenzi wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Gladnes Munuo alisema hayo jijini hapa jana wakati wa uzinduzi wa ripoti ya pili ya utafiti kuhusu unyanyasaji na ukatili wa kijinsia.

             Alisema kwa mujibu wa Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilala, Willy Sangu ubakaji ulipungua mwaka 2013 lakini katika robo ya kwanza ya mwaka 2014 uliongezeka ambapo idadi ya waliohudumiwa katika hospitali ya Amana baada ya kufanyiwa ukatili wa kijinsia ni 310.

              Alisema kwa mujibu wa Ofisa Ustawi wa Jamii wa Kituo cha ‘One Stop Centre’ kilichopo katika hospitali hiyo, Eva Mbilinyi vitendo vya ubakaji vipo kwa kiwango cha juu hali inayodhihirishwa na takwimu za wanaohudumiwa katika kituo hicho.

               Alisema tangu kituo hicho kizinduliwe mwaka jana kimepokea matukio 253 ya unyanyasaji wa kijinsia ambapo kesi 35 zilifikishwa mahakamani hadi Juni 10.
Na (Awadh Ibrahim wa Mjengwa Blog/Kwanza Jamii Radio)

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …