MSANII HUYU MPYA WA FILAMU ZA BONGO ATABIRIWA KUWA TISHIO KWA WAKONGWE

Kila kukicha katika tasnia ya filamu bongo kumekuwa kukichipukia wasanii wapya ambao wamekuwa wakileta mapinduzi kwa wakongwe wa tasnia hiyo kwa namna moja ama nyingine.

Hali hiyo imekuwa ikileta ladha tofauti tofauti kwa watazamaji na wadau mbalimbali hasa wakiona vipaji vipya



Msanii ajulikanaye kama Judith ambaye kwa jina la kisanii anajiita Juddy ni msanii chipukizi ama niseme ni mpya kabisa katika fani ya maigizo Bongo na ameshafanya muvi moja ambayo anadai itakuwa sokoni hivi karibuni

Cha kushangaza zaidi kwa mrembo huyo ni kwamba kisura anafanana sana na super star Irene Uwoya kama ukiangalia picha hizi za Judy na hii inaashiria na yeye atakuja kutisha katika filamu za bongo

Amesema anavutiwa sana na Nisha pamoja na Shamsa Ford ambao amesema levo zao ni za kutisha na wanampa mzuka na yeye wa kukomaa kama wao



Juddy ameamua kuwa muigizaji wa kike wa filamu kwa kuwa ni kazi anayoipenda na pia aje kuwa msanii mkubwa hapa nchini na nje ya nchi na lengo lake pia ni kuinua wasanii wachanga ili nao wakue kisanii

Kwa sasa amesema anaomba sana mashabiki kumpokea kwa mikono miwili na anaimani hatawaangusha, kwani amesema licha ya uzuri wa sura aliopewa na Mungu lakini pia tabia yake pia ni nzuri na atafanya kazi nzuri pia za kisanii


You might also like:

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini