WALIOPOTEZA MAISHA KWENYE KANISA LILILOANGUKA LA TB JOSHUA WAFIKIA 115
Idadi ya
watu waliopoteza maisha kufuatia kuanguka kwa jengo lililopo kwenye
kanisa la TB Joshua jijini Lagos, Nigeria, imefikia watu 115, kwa mujibu
wa serikali ya Afrika Kusini.Waziri
Jeff Radebe wa Afrika Kusini Jumatatu hii ameitaka serikali ya Nigeria
inayokosolewa vikali kufanya uchunguzi juu ya tukio hilo. Tukio hilo
lililotokea Sept 12 kwenye eneo la kanisa la mhubiri maarufu, T.B.
Joshua, limesababisha vifo vya raia 84 wa Afrika Kusini kutoka kwenye
vikundi vya makanisa yaliyomtembelea.Ajali hiyo imesababisha uhasama wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili kubwa kiuchumi barani Afrika.
Waafrika Kusini wamechukizwa na kile wanachokiona kama serikali ya Nigeria inajivuta kufanya uchunguzi juu ya kuanguka kwa jengo hilo na kushindwa kuchukua hatua za haraka kuwaokoa waliokuwa
wamenaswa kwenye vifusi.
Joshua na
wafuasi wake wanadai kuwa ajali hiyo ni shambulio linalohusishwa na
ndege ya ajabu iliyokuwa ikipaa juu ya jengo hilo kabla haijaanguka.
CHANZO: BBC SWAHILI
CHANZO: BBC SWAHILI