ANAYEDAIWA KUWA TAPELI WA AJIRA ANASWA



 Jamaa mmoja anayetumia majina ya Baraka, Muba au Martha Peter
amenaswa kwa kujipatia pesa kiudanganyifu akijifanya Ofisa wa Bodi ya Mikopo wa Chuo cha Ardhi kilichopo jijini Dar.Tapeli anayetumia majina ya Baraka, Muba au Martha Peter. Tukio hilo lilitokea Septemba 19 mwaka huu katika Kituo cha Afya cha Kimara baada ya tapeli huyo kumlaghai dada mmoja aitwaye Wema Raymond wakutane hapo kwa ajili ya vipimo vya ukimwi vilivyotakiwa kuambatanishwa katika fomu ya kuomba nafasi ya kazi ambayo awali dada huyo alidai kupatiwa na tapeli huyo. 
Akizungumza na waandishi wetu, Wema alisema alimfahamu tapeli huyo kupitia kwa rafiki yake aliyemtaja kwa jina la Rebecca, ambaye naye awali alipigiwa simu na mtu huyohuyo akimtaka kimapenzi. 
Wema alisema kuwa rafiki yake alimkatalia tapeli huyo, lakini siku chache baadaye alimpigia tena akimwambia kulikuwa na nafasi ya kazi katika Chuo cha Ardhi hivyo anamhitaji yeye kwa ajili ya nafasi hiyo. 
“Kwa sababu Rebecca ana kazi yake tayari aliamua kunitaarifu mimi kwa kuwa anajua natafuta kazi,” alisema Wema.Alisema alikutana na jamaa huyo ndani ya Chuo cha Ardhi na kupatiwa fomu aliyoelekezwa kujaza kisha akatakiwa kutoa shilingi 280,000 kama malipo ya fomu hiyo na gharama za mafunzo ya siku tatu ya vitendo kuhusu kazi, fedha ambazo hakuwa nazo kwa muda huo na kulazimika kumuomba rafiki yake Rebecca amsaidie.
Wema Raymond aliyetapeliwa na tapeli huyo anayefahamika kwa jina la Baraka au 'Muba'. “Baada ya kumaliza mazungumzo pale chuoni akanisindikiza hadi nje, lakini cha kushangaza pale mlangoni nikamuona anampatia mmoja wa walinzi hela, nikamuuliza kwa nini aliwapa hela, akasema eti watu wengi wanaitaka nafasi ile wakiwemo walinzi hao, hivyo alikuwa akiwapoza wasimsemee kwa kunitafutia mimi kazi isije akafukuzwa kazi,” alisimulia Wema na kuongeza kuwa alitakiwa kesho yake kupima VVU ili vipimo hivyo viambatanishwe kwenye barua yake ya maombi. 
Katika Kituo cha Afya Kimara, alikutana tena na tapeli wake, aliyeonekana kuwasalimia madaktari na manesi kana kwamba wanajuana kisha akaingia kwa dokta na kuzungumza naye.Baada ya muda tapeli huyo alitoka nje kisha akamwambie Wema aingie kwa daktari kwa ajili ya kujaziwa fomu hizo kienyeji bila kupimwa maambukizi ya ukimwi. “Nikiwa ndani machale yalinicheza, ikibidi nimuulize yule daktari kama anajuana na yule jamaa, daktari akasema kwamba hawafahamiani hata kidogo jambo lililonishtua. “Nikamnong’oneza kuwa nahisi kutapeliwa, akaniambia nikakae naye nikijifanya namuongelesha huku yeye akizunguka kwa mlango wa nyuma na kuwaita mapolisi.
Kamanda Suleiman Kova. “Katika upekuzi alikutwa na zile pesa zangu za jana zikiwa kwenye simu yake na shilingi 90,000 akiwa nazo mfukoni huku akionekana kutumia simu yenye jina la Martha Peter ambalo mwenyewe alikiri kuwa alikuwa akinitapeli.” 
“Polisi walichukua maelezo yangu na kufungua jalada RB/4969/2014 KUJIPATIA PESA KIUDANGANYIFU kisha wakaniambia nifike kesho yake,” alisema Wema na kuongeza kuwa siku ya pili alipofika kituoni hapo aliwakuta watu wengine waliodai kutapeliwa na jamaa huyo kwa majina tofauti na walipopiga hesabu fedha alizowatapeli kwa pamoja zilifikia sh.1,435,000.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …