AJALI MOSHI: MUENDESHA BODABODA AGONGWA NA GARI!
Dereva wa pikipiki aliyefahamika kwa jina moja
la Temba anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 25 hadi 35 amenusrika kupoteza
maisha akiwa na mteja wake baada ya kugongwa na gari la kampuni ya ulinzi la
Security Group Africa mjini Moshi mapema leo.
Tukio hilo limetokea majira ya 2:45 asubuhi katika barabara ya Boma Road mjini Moshi likihusisha bodaboda yenye namba za usajili T 587 CYR aina ya boxer na gari lenye usajili nambari T 708 BAF aina ya Nissan.
Gari hilo la kampuni la ulinzi lilikuwa likiendeshwa na dereva aliyefahamika kwa jina la Leornad Essau (34) aliyekuwa akitokea mzunguko wa Arusha kuelekea Voda House mjini humo. Mashuhuda wa tukio hilo walisema gari hilo la ulinzi lilikuwa mwendo kasi mbele yake kulikuwa na bodaboda ilikyokuwa ikimwonyesha ishara ya kupinda kulia ikitokea upande wa kushoto ndipo ilipomgonga kwa nyuma na kusababisha ajali hiyo.

Mashuhuda hao
waliongeza kusema madereva wa kampuni hilo wamekuwa na tabia ya kukimbiza
magari yao pasipo kuwa na sababu za msingi ikiwemo kuwahi kunywa chai na mihogo
ambayo hupikwa karibu na eneo la Voda House.
“Yaani hawa madereva kila siku asubuhi wamekuwa na mashindani kama ya magari (motor rally), unafikiri wanawahi tukio fulani kumbe wala, ni kuwahi kunywa chai na mihogo hapo voda house” alisema shuhuda mmoja.
Dereva wa Bodaboda alikimbizwa katika hospitali ya KCMC kwa matibabu zaidi huku abiria wake mwenye jinsi ya kike (anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 22 hadi 30) akikimbizwa katika hospitali ya Kilimanjaro kwa matibabu zaidi.