MKUU WA MKOA WA MBEYA AIAGIZA SUMATRA KUANGALIA MIKATABA YA MADEREVA
NA KENNETH NGELESI,MBEYA
MKUU wa Mko wa Mbeya Abbas Kandoro ameiagiza Mamlaka ya Udhibiti na Usafiri wa nchi
kavu na majini (Sumatra) kuanza kukagua mikataba ya ajira kwa madereva
kwani wengi wao hujiingiza katika vitendo hivyo ,hawana ajira na hufanya
hivyo kama njia ya kuongeza vipato vyao.
Kandoro amefikia hatua ya kutoa agizo hili ikiwa ni siku tatu
baada ya kuzinduliwa wiki ya usalama barabarani, siri ya kukithiri kwa
ajali akisema kuwa kuna mawakala wanaokatisha tiketi katika vituo vya
mabasi huwalipa motisha ya fedha madereva ili wawahi kufika mapema, hali inayochochea ongezeko la ajali hizo nchini.
Akizungumza
katika kipindi cha tuongee asubuhi, habari kuu, kinachorushwa na kituo
cha televisheni cha Star Tv cha Jijini Mwanza, Kandoro alisema kwamba
mawakala hao wamekuwa wakitoa fedha hizo kwa madereva wakiamani kuwa
gari likifika mapema katika vituo litakuwa likipendwa na abiria.
Alisema kuwa utafiti tulioufanywa katika vituo vya mabasi katika majiji la Mbeya na Dar
es salaam unaonesha kuwa kuna mawakala wanaokatisha tiketi huwapa
motisha ya fedha madereva (maarufu kwa jila la day waka) kwa kwanawapa motisha .
‘Kwasababu wanaamini kuwa gari inayofika mapema inaonekana miongoni mwa abiria kuwa ni gari inayoaminika, imara inayoweza kuwafanya wafanikishe kusafiri kwa haraka na kuwahi shughuli zao za biashara” alisema Kandoro.
Hata hivyo, alisema vitendo hivyo havikubaliki na kuwataka wananchi na wadau wa usafiri nchini kutoa taarifa za siri ili kuwafichua watu hao wanaoendekeza vitendo hivyo vinavyohatarisha na kugharimu maisha ya watanzania .
Kuhusu agizo la Sumatra kukagua mikataba ya madereva, Kandoro alisema kuwa hali hiyo inaweza kwa kiasi kikubwa kuwadhibiti wa wamiliki wa magari kuacha
tabia iliyozoeleka ya kuifanya sekta ya usafirishaji ya holela na
kusababisha madereva kufanya mambo ya hovyo yanayohatarisha maisha ya
watu.
Kandoro alisema kuanzia Januari hadi Septemba 10 mwaka huu jumla ya ajali kwa
mwaka huu kuanzia Septemba jumla ya ajali 297 zilitokea mkoani Mbeya na
kusababisha vifo vya watu 210, huku majeruhi ambao baadhi yao wamepata
ulemavu wa kudumu wakiwa 402.
“Sasa
hali inaonekana kama haitachukuliwa jitihada za makusudi kudhibiti
mambo yatakuwa mabaya zaidi, kwani ndani ya mwezi huu wa Septemba pekee jumla ya ajali zilizotokea ni 16 na kusababisha vifo 11 na majeruhi 15” alisema Kandoro.
Wiki
iliyopita Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Kandoro alifanya ziara ya kushtukiza
majira ya saa 11:00 alfajiri katika kituo kikuu cha mabasi Mbeya na
kuzungumza na abiria, madereva , mawakala wa kukatisha tiketi na wapiga debe akiwaasa kufuata taratibu ili kuthibiti wimbi la ajali.
Hata
hivyo kauli hiyo ya Kandoro imekuja ikiwa siku chache tangu Mwenyekiti
wa chama cha madereva wa mikoani (TDA), Protas Mpora, alisema changamoto nyingine inayochangia ongezeko la ajali ni madereva wengi kutokuwa na sifa kutokana mfumo wa sekta hiyo kutokuwa na mfumo mzuri.