WAGANGA WANAWEZA KUFANYA WATU KUWA MATAJIRI LAKINI WAO WANABAKI MASIKINI: BOFYA HAPA KUJUA SIRI


Kuna watu ambao wanapata mafanikio makubwa kwa kutumia uchawi. Ila mafanikio yale hayaletwi na uchawi bali imani ya mtu husika.

Tutajadili kwa nini waganga wanaweza kuwapatia watu wengine dawa au mbinu za kuwa matajiri wakati wao ni masikini. Na pia tutaangalia jinsi ambavyo unaweza kutumia mbinu hizi wanazotumia waganga bila ya wewe kuwa mchawi na ukafikia mafanikio makubwa.

Kila mmoja wetu anaelewa kwamba kuna watu wanakwenda kwa waganga na wanasaidiwa kupata utajiri. Japokuwa utajiri huu haudumu, lakini angalau wanaupata kwa kiwango fulani.

 Wakati waganga hawa wanawasaidia watu kuweza kujenga magorofa, wao bado wanakaa kwenye vibanda vya nyasi.

Sasa kwa nini wao wasingetumia uchawi wao na kuwa matajiri zaidi ya hao wateja wao? Ina maana wao hawapendi utajiri huo?

Mbinu za waganga kuwasaidia watu kupata utajiri.
Watu wanaokwenda kwa waganga ili kupata utajiri au mafanikio yoyote hupewa masharti ambayo ni magumu kwa kiasi fulani.

Na watu hawa huambiwa wakivunja masharti hayo tu utajiri wao unaisha mara moja. Ni masharti haya ambayo humjengea mtu nidhamu kubwa sana na kumfanya aweze kufanya kazi kwa juhudi kubwa kuliko wengine ambao wanafanya anachofanya.

Kwa mfano mganga anamwambia mtu kila siku aamke asubuhi na mapema sana na apasue nazi barabarani ndio aende kwenye biashara zake.

Kupasua nazi hakuna uhusiano wowote na mafanikio yake ila kuamka asubuhi na mapema kila siku ina msaada mkubwa kwenye mafanikio yake.

Hivyo mtu huyu atafuata masharti haya kila siku na hata kama kuna siku hajisikii itambidi afanye tu kwa sababu ameshaaminishwa akiacha atafilisika.

Sasa wewe ambaye huna sharti la aina hii siku ukiwa hujisikii vizuri unalala, siku nyingine unachelewa na hivyo kushindwa kufikia mafanikio makubwa.

Masharti mengine kama kutokufanya starehe, kutokunywa pombe, kuvaa nguo moja na mengine mengi yanapelekea mtu kupunguza matumizi na kupata muda mwingi wa kufikiria kazi au biashara yake.

Masharti mengine yanayotolewa na waganga ni kumfanya mtu aweze kuondoka kwenye woga wake(comfort zone). Kila mmoja wetu kuna vitu fulani anaogopa kufanya, lakini vitu hivi ndio vinaweza kumletea mafanikio.

 Ili kukuondolea woga huu mganga anamfanya mtu afanye jambo kubwa sana ambalo litamuondolea woga kabisa.

 Kwa mfano mtu anaambiwa aue, kwa kuona kwamba ameweza kuua mtu, inamfanya mtu asizuiwe na kitu chochote.

Kikubwa ambacho mganga anamsaidia mtu ni kumjengea utaratibu ambao lazima kila siku ataufuata na pia kumjengea nidhamu binafsi na hivyo kuweza kufanya jambo hata kama hajisikii kufanya. Na hili ndio hitaji kubwa la kuweza kufikia mafanikio.

Kwa nini waganga hawawezi kutumia mbinu hii wenyewe.?
Kwa sababu wanajua inavyofanya kazi na pia hawana mtu wa kuwajengea imani hiyo kubwa kwao wenyewe.

Kwa nini watu baadaye hufilisika?
Wengi hufilisika baadae kwa sababu wanapopata mafanikio wanasahau kutumia yale masharti waliyopewa na pia imani yao inakuwa imewekwa kwenye vitu fulani(mfano hirizi) badala ya kuwa kwao wenyewe.

Ufanyeje ili uweze kutumia mbinu hii kufikia mafanikio.
Cha kwanza kabisa lazima ujijengee nidhamu binafsi. Jiwekee masharti yako ambayo utayafuata kila siku na hakikisha unayafuata.

Kwa mfano weka utaratibu kwamba kila siku utakuwa unaamka saa kumi asubuhi, kuipanga siku yako na kisha kujisomea kidogo.

Baada ya hapo unawahi kwenye eneo lako la kazi au biashara na kuanza kazi zako mapema. Pia unaweza kujiwekea utaratibu kwamba kila mteja au mtu yeyote unayekutana naye kwenye siku husika atajisikia vizuri kukutana na wewe.

Fuata masharti haya kila siku na utaona mabadiliko makubwa kwenye maisha yako na shughuli zako.

Kwa hiyo mpaka sasa una mbinu mbili za uhakika za kufikia mafanikio;
1. Una uwezo mkubwa uko ndani yako, ila unatakiwa kuwa na imani kubwa sana kwamba unaweza kupata kile unachotaka.

2. Lazima uwe na nidhamu binafsi, uwe na masharti(rituals) na uwe na utaratibu wa kufanya kila siku (routine). Vitu hivi jiwekee mwenyewe na vifuate kila siku kwenye maisha yako.

Ukiweza kufanya mambo hayo mawili ni lazima utafikia mafanikio makubwa.

Nakutakia kila la kheri katika kufikia mafanikio. Kumbuka unaweza kufanikiwa kwa kiwango kikubwa sana bila ya kutumia uchawi au kwenda kwa mganga.Uchawi kamili upo kwenye kichwa chako. Anza kuutumia sasa.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini