MAPENZI SUMU, MKE WA MTU AMFUNDISHA ADABU HAWARA


Mama mmoja almaarufu kwa jina la Mama la Mama anadaiwa kumbonda hawara wa mumewe baada ya kumwekea mtego wa fumanizi kwenye nyumba ya kulala wageni (gesti).

Sekeseke hilo kubwa na la aina yake lililoshuhudiwa na wanahabari wetu lilijiri wikiendi iliyopita kwenye Gesti ya White Paris iliyopo eneo la Kimara-Kona jijini Dar na kusababisha umati (inzi) kujazana na kufunga mtaa.
 
Habari zilidai kwamba Mama la Mama alihisi mumewe anachepuka hivyo aliamua kumfuatilia nyendo zake hasa kwenye kipengele cha matumizi ya simu.Ilisemekana kwamba, Mama la Mama alichukua laini ya simu ya mumewe alipokuwa akijiandaa kwenda kazini.
Hawara akihaha ndani ya gesti ya White Paris (kimara) mara baada ya fumanizi.
Ilidaiwa kuwa baada ya mumewe kuondoka na simu bila kujua haina laini, Mama la Mama aliiweka laini hiyo kwenye simu yake kisha akapitia namba kadhaa na kuitilia mashaka moja na alipopiga, akawa amepatia.Akamhadaa kwa kubadilisha sauti na kuzungumza kama mumewe.
 
Habari zilizidi kunyetisha kuwa baada ya kubadili sauti alifanikiwa kumwingiza mwanamke huyo mkenge lakini hawara huyo akamuuliza kulikoni ‘baby’ sauti imebadilika ndipo akamjibu anaumwa.

Ilielezwa kwamba Mama la Mama alimdanganya hawara huyo kuwa endapo wataonana atapona hivyo akamwambia wakutane gesti hiyo kwa kuwa Mama la Mama ni mkazi wa Kimara, Dar.Ilisemekana kuwa Mama la Mama, huku akijifanya mwanaume alimuomba hawara huyo wakutane gesti kwani alikuwa amekumbuka penzi lake.
 
Ilidaiwa kwamba, bila kufikiria mara mbili, hawara huyo alikurupuka, akafunga safari kwa kuwa aliahidiwa penzi na fedha za kujikimu.Ilisemekana kwamba baada ya makubaliano Mama la Mama alikwenda kwenye gesti hiyo na kulipia chumba kisha akamsubiri kimwana ambaye alikuwa akitokea eneo la Kigogo, Dar.

Habari zilitiririka kuwa baada ya kufika kwenye chumba alichoelekezwa ndani ya gesti hiyo alishangaa kukuta aliyemuita ni mwanamke mwenzake ambapo alijikuta akiishiwa nguvu na kupigwa na butwaa.
 
Wanahabari wetu wakiwa eneo la tukio, walimwona mrembo huyo akiwa amechanganyikiwa na hapo ndipo sekeseke likaanza na kujaza kadamnasa ndani na nje ya gesti.
 
Mama la Mama alishuhudiwa akimbonda mwanamke huyo kwa madai kwamba amekuwa akimzuzua mumewe na kumfanya ashindwe kutulia kwenye ndoa.

Baada ya sekeseke zito, hawara huyo aliogopa kutoka nje ya gesti akihofia kupokea kipigo kutoka kwa raia wenye hasira kali waliokuwa wamezagaa nje hivyo aliamua kukodi chumba kingine ambapo alizama chumbani kisha kujifungia kwa ndani na kulala.
 
Akiwa kwenye mishemishe zake bila kutambua lolote, mwanaume aliyesababisha wanawake hao kukutana aliendewa hewani na mkewe na alipoulizwa kama anamfahamu mwanamke aliyeitwa gesti alijibu kuwa aliwahi kuwasiliana naye walipokutana baa kwani ni baamedi.

Awali kabla ya kujifungia chumbani, hawara huyo alidai kuwa mume wa Mama la Mama ni mpenzi wake ambapo wamedumu kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa takribani mwezi mmoja.
 
Alisema kwamba kilichomtokea anamwachia Mungu kwani amedhalilika kupita maelezo.
Credit:Gpl

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini