AUAWA NA WANANCHI BAADA YA KUMUUA MKEWE WILAYANI MPWAPWA MKOANI DODOMA
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi DAVID
MISIME – SACP akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani
Na. Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.
Watu wawili wameuawa Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma katika matukio mawili tofauti.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi DAVID
MISIME – SACP amesema tukio la kwanza limetokea mnamo tarehe 20/09/2014
majira ya saa 23:30hrs katika Kijiji cha Mzogole Wilayani Mpwapwa Mkoani
Dodoma ambapo mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la MWAJUMA D/O CHOMOLA
mwenye umri wa miaka 48, Mgogo mkazi wa Mzogole aliuawa kwa kupigwa na
Rungu tumboni upande wa kushoto na mumewake aliyefahamika kwa jina la
RICHARD S/O KODI mwenye umri wa miaka 55, Mhehe mkulima na
mkazi wa kijiji cha Mzogole Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma ambaye nae aliuawa tarehe 21/09/2014 majira ya saa 09:00hrs baada ya kushambuliwa na wananchi waliojichukulia sheria mkononi na alifariki dunia akiwa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa baada ya wananchi hao kupata taarifa kuwa mwanamke huyo kafariki kutokana na kipigo cha mume wake.

MISIME amesema uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha mauaji hayo
ni wivu wa mapenzi kwani RICHARD aliuawa na wananchi baada ya kumuua
MWAJUMA ambaye alikuwa mkewake aliyekuwa akiishi nae, baada ya kuchelewa
kurudi kutoka kwenye sherehe iliyokuwa hapo kijijini akidhani kuwa
ameenda kwenye masuala mengine.
Aidha Kamanda MISIME amesema wananchi waliojichukulia sheria mkononi bado wanatafutwa ili wafikishwe mahakamani.