MAJONZI NA SIMANZI: JWTZ MILIONEA ALIVYOUAWA KWA RISASI.
NI taharuki iliyojaa majonzi na simanzi kufuatia Jeshi la Wananchi wa
Tanzania ‘JWTZ’ Kikosi cha CMTU jijini Dar kuondokewa na mpiganaji
wake, Sajenti Yohana Lugendo Gweso (40) ambaye alikuwa milionea
aliyepigwa risasi sita mwilini na kufariki dunia papo hapo.
Mwili wa marehemu Sajenti Yohana Lugendo Gweso (40) wa Jeshi la
Wananchi wa Tanzania ‘JWTZ’ Kikosi cha CMTU ukiwa kwenye jeneza. Tukio
hilo la kusikitisha, lilijiri saa 1:45 usiku wa Septemba 22, mwaka huu,
Ukonga Babana ndani ya baa maarufu ijulikanayo kwa jina la Super Karatu.
UWAZI HATUA KWA HATUA
Kufuatia tukio hilo, Uwazi kama kawaida yake lilifuatilia kwa kina ili kubaini yaliyofichika nyuma ya pazia kama siyo sirini!
Ikadaiwa kuwa, baada ya kupata simu hiyo alifika kwanza nyumbani
kwake Gongo la Mboto kambini.“Alipofika alikula chakula cha mchana kisha
alipumzika. Ilipofika saa 11 jioni aliondoka kwenda kwenye shughuli
zake za biashara. “Alipokuwa huko inadaiwa alipigiwa simu na mtu huyo wa
mwanzo na kupanga sehemu ya kukutania ambapo ilikuwa ni hapo baa,”
alisema ndugu mmoja akiomba kusitiriwa jina lake.
Mpiganaji huyo inadaiwa wakati anatoka katika biashara zake alikuwa
na mtoto wa dada yake aliyetajwa kwa jina moja la Frank ambaye alikuwa
akisimamia hesebu zote za biashara. Siku hiyo walikuwa wamekusanya kiasi
cha shilingi milioni 42.
Ikadaiwa kuwa, walipofika Banana kabla ya kuingia Baa ya Super
Karatu, marehemu ambaye alikuwa akiendesha gari lake aina ya Toyota
Prado lenye namba za usajili T 855 BWK, alimshusha Frank na kumtaka
atangulie nyumbani kwani alihitaji kwenda Super Karatu kukutana na
mwanamke huyo ambaye baadhi ya watu wanadai ni mweupe, mnene aliyepanda
hewani (mrefu).
Habari zaidi zinasema kuwa, marehemu aliwasili kwenye baa hiyo saa 1
usiku na kutafuta maegesho. Alishuka na kuanza kutembea, lakini ghafla
kwa nyuma aliitwa na watu wawili ambao walimuita; “Gweso tuko hapa.”
Wakati anageuka kuwafuata watu hao, watu wengine walianza kuvunja gari lake vioo hivyo alirudi mbio ili kujua nini kinaendelea.
“Kumbe wau hao walikuwa kundi moja na mashambulizi ya risasi yalianzia hapo.
“Marehemu alimiminiwa risasi sita mwilini, alipigwa kichwani,
nyingine kifuani na walimchukulia fedha zote milioni 42 na bastola yake
kisha wakatokomea,” aliendelea kusema ndugu huyo.
Baada ya tuko hilo ndugu, jamaa na marafiki walijulishwa kuhusiana na
kifo cha mjeshi huyo ambapo walifika na kuuchukua mwili wa marehemu
hadi Hospitali ya Rufaa ya Lugalo jijini Dar kwa ajili ya kuuhifadhi.
UTAJIRI WA MAREHEMU
Mpaka kifo chake, marehemu Gweso alikuwa akimiliki magari manne ya
kisasa,Toyota Prado (alikuwa nalo siku ya tukio), Toyota Verossa, Suzuki
Vitara na VRS.
Aidha, alikuwa akimiliki biashara mbalimbali kama vile baa, duka la
bia za jumla na nyumba ya kulala wageni. Vyote vipo Ukonga, Dar.
ALIANZA KUWINDWA MWAKA 2008
Habari zaidi zinadai kuwa, marehemu alianza kuwindwa mwaka 2008
ambapo watu wasiojulikana majina, sura wala nia yao, walivamia nyumbani
kwake, Banana (uswahilini) na kumpiga risasi mtoto wa dada yake na
kufariki dunia papo hapo.
MAZISHI YAKE
Marehemu Gweso amezikwa Septemba 27, mwaka huu katika Makaburi ya
Kijiji cha Tailo Wilaya ya Bunda Mkoani Mara. Ameacha mke mmoja na
watoto wanne.