UTINGO WA LORI AGONGWA NA KUFA PAPO HAPO WILAYANI MAKETE WAKATI AKIMUONGOZA DEREVA WAKE KUPITA
Askari wakiwajibika.
Lori lililosababisha ajali.
Hali
ya simanzi imetawala miongoni mwa wakazi wa Makete mjini mkoani Njombe
kufuatia utingo wa lori lililobeba skaveta kugongwa na lori hilo hadi
kufa papo hapo
Tukio
hilo limetokea jana majira ya saa 11:45 alfajiri wakati lori hilo
likipita kwenye eneo lililolundikwa vifusi kufuatia matengenezo ya
barabara hiyo kwa kiwango cha lami
Akizungumza
na eddy blog mkuu wa polisi wilaya ya Makete Bw. Alfred Kasonde
amemtaja marehemu kuwa ni Albert Mwalukasa (21) ambaye amegongwa na lori
hilo lenye namba za usajili T 489 BDW mali ya Timoth Mwalukasa mkazi wa
mkoa wa Mbeya
Lori
hilo lilikuwa likiendeshwa na Bw. Lewad Mekule ambaye kwa sasa
anashikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano zaidi na upelelezi tayari
umekamilika hivyo atafikishwa mahakamani kujibu mashitaka ya mauaji
yanayomkabili
Mwili
wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia Maiti cha
hospitali ya wilaya ya Makete ukisubiri ndugu wa marehemu waliopo mkoani
Mbeya kufika kuuchukua kwa ajili ya taratibu za kumzika
Baba
mdogo wa marehemu aitwaye Allan Mwalukasa ambaye alikuwepo kwenye lori
hilo amesema hata yeye anashangaa kilichopelekea kifo cha ndugu yake
kimetokeaje
"Nilikuwa
mbele hapa naangalia sehemu ambayo kidogo ni nzuri kwa ajili ya vifusi
hapa ambavyo vimelundikwa barabarani ghafla nkashangaa nimesikia kelele
nyuma huko analia aaaaah nikashindwa kuelewa, kuja kukimbia ninamkuta
yupo chini ya gari, huyo ni mtoto wa kaka yangu ambaye tumefuatana"
amesema Mwalukasa
Kwa
upande wa wananchi waliofika eneo la tukio wamesema marehemu alikuwa
akimuongoza dereva namna ya kupitisha lori kwenye vifusi vilivyolundikwa
muda mrefu barabarani bila kusambazwa, lakini ghafla aliteleza kwa kuwa
alikuwa akipita juu ya vifusi hivyo ndipo alipogongwa na kufariki papo
hapo
Wananchi
hao wametupa lawama kutokana na vifusi hivyo kukaa muda mrefu bila
kusambazwa hali inayopelekea usumbufu kwa watumiaji wa barabara hiyo, na
hivi karibuni mwandishi wetu alizungumza na mkandarasi wa ujenzi huo
ambaye alisema amekwenda Morogoro kufuata vifaa vya kumalilisha ujenzi
huo
Hata hivyo wameshauri barabara mbadala zilizojengwa na mkandarasi huyo zitumike ili kuepusha madhara zaidi
Na Eddy Blog