Wolper afunguka kuwa sasa yupo tayari kuwa mke
Staa mkali wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper |
STAA mkali wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper amefunguka kuwa kwa sasa yuko tayari kuolewa kwani anaamini anastahili kuwa mke.
Wolper alisema, katika
maisha siku zote anaamini kuna kipindi kinapita cha kufanya ujana
ambacho tayari ameshakipitia na sasa ni muda wa yeye kutengeneza
familia.
“Naamini kabisa huu sasa
ni muda muafaka kwangu, niko tayari kabisa kuwa mke maana nimepitia
vitu vingi ambavyo mara nyingi wengi wao huwa wanakimbilia kwenye ndoa
wakiwa bado hawajavimaliza halafu mwisho wa siku wanazishindwa, mimi
nishamaliza vyote,” alisema Wolper pasipo kufafanua kama tayari
ameshampata mchumba au la.
Jacqueline Wolper |
Wolper amewahi kuwa
katika uhusiano wa kimapenzi na mastaa kadhaa akiwemo Mohamed Mtoro
‘Dalas’ ambaye alimbadilisha dini ili waweze kufunga ndoa lakini ikaota
mbawa.