DROGBA WA PORI LA SELOUS ANAYEJIPATI MKWANJA MREFU KUTOKA KWA WAZUNGU KILA SIKU Drogba 1
KATIKA
kipindi cha miaka minne iliyopita hadi kufikia leo, watalii wanaoenda
kutembelea Pori la Akiba la Selous lililopo katika Kijiji cha Mloka
kilichopo Kata ya Mwaseni wilayani Rufiji mkoani Pwani, wanapata fursa
ya kufurahia utalii wa aina yake pindi wanapokutana na mmoja wa
wanakijiji wa eneo hilo anayejulikana kwa jina la Mwananyika lakini kwa
sasa amepewa jina la Drogba kutokana na umaarufu aliojipatia miaka ya
hivi karibuni. Inaelezwa kuwa amefanana na Drogba yule mwanasoka
anayechezea timu ya Chelsea kwa sasa.
Imeelezwa kuwa, Kijiji hiki ni kijiji cha
mwisho kabisa kabla ya kufika kwenye geti la Mtemere, moja ya mageti ya
kuingilia kwenye pori hili. Watalii kutoka ndani na nje ya nchi
(hususani raia wa kigeni) wanapofika katika kijiji hiki hukutana na
Drogba ambaye inaelezwa kuwa amepata umaarufu mkubwa kuanzia mwaka 2011
hadi sasa.
Wenyeji wa kijiji hiki wanasema Drogba ni
mmoja wa wajasiriamali aliyewekeza nguvu na uelewa wake wa mambo ya
wanyama pori na mazingira yao kwa kutoe elimu kwa wageni wanaungana naye
katika kuelewa tabia za wanyama. Yeye haingii kwenye hifadhi bali
anazunguka nje ya pori hili kutokana na maeneo mengi kupitika kirahisi
na wanyama kupata nafasi ya kuzunguka katika moja ya vijiji vilivyopo
kijijini humo na maeneo ya jirani.
Yeye safari zake hujulikana kama bush walk na
wageni wake hupata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu
maisha ya mwanakijiji na wanyamapori. Vitu kama dawa mbalimbali za
asili, hadithi za kale huwa ni sehemu ya vitu wanavyojifunza wageni wa
‘Drogba’.
Shughuli za Mwananyika au Drogba
Watumiaji wa njia inayoelekea katika geti
hilo wanaeleza kuwa moja ya shughuli anazofanya Drogba ni kuelekeza
wageni kwenye matembezi wanaoingia kwenye pori hilo na kujipatia kipato
cha kuendeshea maisha yake pamoja na familia yake (anatumia lugha tatu
hadi sasa, Kiswahili, Kiingereza na Kifaransa).
Mwenyewe hujigamba kwa kuziita true Africa walking safari na
anapokuwa kazini huwa anavaa mavazi ya asili kabisa (baadae huvaa
mavazi ya kawaida) ambayo huyatengeneza kwa magome ya miti huku akiwa
amebeba ngao, mkuki na kikapu chake cha kubebea mitishamba na vitu
vingine anavyoweza kuvipata akiwa katika eneo lake la kazi pia
anazunguka kwenye barabara zilizopo kando kando na pori hilo na wakati
mwingine hulazimika kuingia kwenye baadhi ya mapori na kuzunguka na
wageni wake nje ya hifadhi japo wapo wanyama (wakali na wapole) wapo
katika maeneo anayotembelea.
Kwa ajili ya tahadhari na usalama anapofanya safari za miguu na wageni wake siku zote huwa anaambatana na Askari wa hoteli (campsite) waliofikia wageni wake, askari anakuwa na bunduki kwa ajili ya tahadhari kwa chochote kinachoweza kutokea.
Mara zote mgeni anayefanya utalii katika
pori hili, husindikizwa na askari wa Maliasili na wakati huo Drogba yeye
anaendelea kuzunguka nje ya hifadhi bila kuwa na woga.
Safari zake huwa na vituo vingi ndani
yake na kwenye kila kituo kuna jambo ambalo huona ni vyema wageni wake
wanastahili kulifahamu na pia endapo mnaweza kukutana na wanyama
anatumia nafasi hiyo kuwafundisha wageni mazingira ya wanyama.
Miongoni mwa mambo wageni wanayofaidi
wanapokuwa na Drogba ni kufundishwa namna ya kutambua nyayo za wanyama
mbalimbali ambazo huwa wanakutana nazo wakiwa safarini.
Historia yake kwa ufupi
Hadi sasa ukifika kijiji hicho kama
mtalii ukasikia watu wanamzungumzia Drogba basi kuna uwezekano mkubwa
wakawa wanamzungumzia Drogba wanayemjua wao anayetembeza wageni
wanaotoka ndani nan je ya nchi. na sio yule ambaye watu mbalimbali
wamemzoea kumsikia (anayechezea timu ya Chelsea).
Kwa hivi sasa watu wengi wanaeleza kuwa
hata jina lake kamili hawalijui kutokana na umaarufu aliojipatia (ni
mmoja kati ya watu maarufu sana kijiji hapo) na hususani kwa wadau wa
utalii ambao hupeleka wageni kwenye pori hilo kupitia lango la Mtemere
linalopakana na kijiji cha Mloka ambapo wanyama hutoka nje na kuzunguka
vijijini na maeneo ya karibu.
Hali hii inawafanya wageni kufanya
kutembelea maeneo ya nje ya pori ambazo huwaleta karibu na wanyama wa
porini, baadhi ya wanyama wanaopatikana nje ya pori hilo ni Swala,
Nyati,Tembo, Twiga na Viboko, na wanyama wengineo ambao huonekana katika
maeneo ambayo Drogba hupendelea kuzunguka akiwa na wageni wake.
Ni nadra sana kuweza kumsogelea Twiga
mpaka muwe na usawa wa karibu mara nyingi Drogba yeye anamkaribia bila
Twiga kutimua mbio. Inaelezwa kuwa mara chache Twiga huvumilia kwa muda
kidogo na baadae kuanza kulala akiwa na Drogba.
Unapoanza kukiacha kijiji cha Mloka na
kisha kuelekea lilipo geti la kuingilia Selous (Mtemere) utaanza
kukutana na vibao vikikuonyesha zilizopo kambi kadhaa. Kambi nyingi za
Mloka zimejengwa pembezoni mwa mto Rufiji ukiwa unaelekea Mtemere nyingi
zipo upande wa Kushoto wa barabara. KARIBUNI SANA