MCHEZAJI AFARIKI HUKO UGANDA KUFUATIA BAO LA FRANK LAMPARD
Fahad
Musana, ambaye ni shabiki wa kutupwa wa klabu ya soka ya Chelsea,
amefariki dunia baada ya mchezaji wa zamani wa klabu hiyo, Frank
lampard, kuifungia Manchester City bao la kusawazisha, katika pambano
lililopigwa jana baina ya timu hizo mbili.
Musana,
mwenye umri wa miaka 24, na ambaye alikuwa mcheza kandanda la kulipwa
nchini Uganda, alikuwa akitizama mechi hiyo iliyovuta hisia za mashabiki
wengi katika kona mbalimbali za dunia, na alianguka na kuzimia mara
baada ya Lampard kusawazisha bao, ikiwa ni dakika chache sana tangu
aingie kutokea benchi, katika dakika za lala salama.
Alithibitishwa
kuwa amefariki baada ya kuwasili katika hospitali ya kijeshi ya Bombo,
na rafiki wa karibu wa marehemu amenukuliwa na vyombo vya habari akisema
“Jamaa, amekuwa ni shabiki wa kweli wa Chelsea, ambaye angeweza kufanya
lolote lile kwa ajili ya klabu hiyo. Tulifanya naye mazoezi asubuhi ya
jumapili, na hata mchana tukala chakula cha mchana pamoja, hakika
inasikitisha”
Tukio
hili la kusikitisha, limethibitishwa na Shirikisho la vyama vya soka
nchini Uganda (FUFA), ambalo limetoa tamko lake kufuatia mkasa huu wa
kushtusha.
“FUFA,
limekumbwa na mshtuko baada ya kupokea taarifa za kifo cha ghafla cha
mchezaji wa klabu ya Simba ya Uganda, Misana Fahad, katika hospitali ya
Bombo. Mwili wa marehemu bado uko hospitalini hapo, na taratibu za
mazishi zinaandaliwa na taarifa zitatolewa baadae”, sehemu ya taarifa ya
FUFA imesomeka hivyo.
Hii
si mara ya kwanza kwa mashabiki wa soka kufariki kufuatia timu
wanazozishabikia kushindwa kuibuka na ushindi katika mechi zao.
Kumbukumbu za hivi karibuni sana kwa ukanda wetu wa Afrika Mashariki na
Kati, ni za shabiki mwingine wa soka aliyefariki dunia msimu uliopita,
baada ya timu aliyokuwa akiishabikia ya Manchester United kupoteza moja
ya mapambano yake, ilipokuwa chini ya kocha David Moyes