Hospitali imesemaje kuhusu mchezaji wa Uganda aliefariki baada ya goli la Lampard?


Ni taarifa ambayo ilitolewa na vyombo mbalimbali vya habari kwamba mchezaji wa club ya Simba ya Uganda Fahad Musana amefariki kutokana na mshtuko wa goli alilolifunga Frank Lampard wa Manchester City wakati wakicheza na Chelsea juzi.
Pamoja na hayo, taarifa kutoka hospitali kuu Uganda ya Mulago zinasema Fahad alifariki kutokana na ugonjwa wa pnemonia na sio mshtuko uliotangazwa awali ambapo Fahad aliezikwa September 24 2014 baada ya kufia kwenye hospitali ya Bombo Barracks alikua shabiki mkubwa wa Chelsea.

Marehemu ni huyu alievaa jezi ya njano
Kabla ya kifo chake Musana alifanya mazoezi na timu yake Jumapili asubuhi na kula chakula cha mchana na mmoja wa marafiki aitwae Gerald Bagoole na kisha wakati wa mpira alikwenda kutazama jirani na anapoishi.

Habari za kuhuzunisha za mashabiki wa soka Uganda zimekua na mfululizo wake kwenye hii miaka miwili huku wengine wakijiua baada ya kushindwa mechi na mmoja akiwa na majonzi ya nyumba yake baada ya kuiweka rehani akishadadia kutabiri ushindi wa timu yake.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini