NDEGE ZA KIVITA HATARI ZAIDI DUNIANI ZINAZOMILIKIWA NA URUSI

Japokuwa Urusi inaaminika kuwa na silaha nyingi hatari za kivita lakini mtandao wetu kwa msaada wa mtandao wa yahoo.com unakuletea ndege ambazo ni hatari zaidi zinaposhambulia toka angani zinazomikiwa na Urusi.
1.PAK FA 
PAK FA.
PAK FA ina rada maalum ya kivita inayosaidia kutazama muelekeo na kuchunguza umbali mrefu kabla ya kufika eneo husika, licha ya uwezo wa kubeba silaha nyingine pia ina uwezo wa kubeba makombora makubwa sita ikiwa ni pamoja na kutupa toka hewani pamoja na ardhini.
PAK kwa mara iliruka hewani kwa dakika 47 January 29, 2010 na baada ya hapo ilifanyiwa majaribio zaidi ya 450 mwishoni mwa mwaka 2013.
Russia inatarajia kutengeneza ndege kama hizo 400 mpaka 450 kufikia mwaka 2020 au 20140 katika mradi ambao inashirikiana na India iliyochangia kiasi cha dola bilioni 6 ili kufanikisha mpango huo.
2.Su-25 FROGFOOT 
Su-25 FROGFOOT. Picha|digitalcombatsimulator.
Ndege hii ina kasi sana na ina sehemu kumi ambazo zinawekwa mabomu ili kushambulia, pia ina uwezo wa kushambulia hewani kwa hewani ikiwa na maana kutungua ndege nyingine hewani na pia kushambulia toka hewani kwenda ardhini. 
Ndege hii ilitengenezwa maalum kushambulia ikiwa karibu na uwanja wa vita si kutoka mbali pia inabeba makombara.
Ndege hii imeshawahi kushambulia Afghanistan mwaka 1979-1989, vita ya Chechnya na sasa hivi inatumika katika mgogoro wa Ukraine.
3.Tu-95 BEAR STRATEGIC BOMBER
Ndege hii ilitengenezwa maalum kwa kurusha mabomu ya nyuklia lakini imekuwa ni vigumu kwa mabomu hayo kutumika kutokaqna na mpango wa Marekani wa kupinga matumizi ya mabomu hayo hatari Duniani.
Kutokana na kasi yake, ndege hii ilitumika kwenye vita ya baridi kufanya doria kaskazini mwa bahari ya Atlantic pamoja na kuongoza vikosi vya majeshi ya maji. 
Ndege hii kwasasa ipo katika matengenezo ya kuiboresha zaidi kwasababu ilitengenezwa miaka 60 iliyopita.
4.Tu-160 BLACKJACK STRATEGIC BOMBER
Add caption
Ndege hii ilikuwa ni toleo la mwisho mwaka 1980-1992 la Soviet Union kabla haijasambaratika na Russia kumiliki zana nyingi za kivita.
Ndege hii ina uwezo mkubwa wa kufanya shughuli za kivita usiku katika hali zote za hewa huku ikiwa imebeba mzigo mkubwa wa mabomu ya nyuklia pamoja na makombora yenye uzito mkubwa.
Ndege hii ina kasi ya kilomita 2,000 kwa saa pamoja na kutembea umbali wa kilomita 14,000 bila kujazwa mafuta kwa mara nyingine.
Ndege hii pia kutokana na muundo wake ina uwezo wa kugundua kombora lililoelekezwa kwake na kukwepa kabla halijaleta madhara.
5.Su-35 FLANKER FIGHTER
Su-35 FLAKER FIGHTER. Picha presstv.ir.
Ndege hii ina kifaa maalum kinachoweza kumtafuta adui umbali wa kilomita 400 na kumshambulia.
Ndege hii ambayo ina injini mbili pia ina uwezo wa kubeba mzigo mkubwa wa sialaha mbalimbali pamoja na maeneo 14 yanayofungwa silaha kwa ajili ya kushambulia.
*Mpangilio wa namba haumaanishi kuwa iliyo namba moja ndio inaongoza au namba tano ndio ya mwisho.
Chanzo YAHOO

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini