15 PICHAZ: RAIS JK AIFAGILIA MAGEREZA DAY

Rais Dk. Jakaya Kikwete akipokea heshima ya Wimbo wa Taifa mara baada ya kuwasili katika Viwanja  vya Chuo cha Maofisa Magereza kilichopo Ukonga jijini Dar.

Rais JK akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili.
Rais JK akiangalia vikosi mbalimbali vya Jeshi la Magereza.
Rais JK akimpandisha cheo mwanafunzi bora katika kozi ya 21 kutoka Inspekta na kuwa ASP.
Kikosi cha Bendera kikitoa heshima mbele ya Rais Kikwete.
Kikosi Maalum cha Magereza nacho kikitoa heshima kwa Mheshimiwa Rais Kikwete.
Wanawake kutoka Kikosi Maalum cha Magereza nao hawakuwa nyuma, hapa wakitoa heshima zao mbele ya Rais JK wakiwa na silaha aina ya AK 47.
Askari wakiwa wamevaa mavazi yanayofanana ya Askari wa Kikoloni wakipita mbele ya Rais JK. Kikosi hicho kilivuta hisia za watu wengi waliohudhuria mahali hapo.
Kutoka kushoto ni: Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil, Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu, Kamanda wa Vikosi vya Ardhini wa JWTZ, Meja Jenerali Salum Kijuu na Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja wakifuatilia hafla hiyo.
Rais JK (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama.
JK akielekea kukagua mabanda ya maonyesho yaliyoandaliwa na jeshi hilo.
Rais JK akiangalia mchele huku akipokea maelezo kutoka kwa ofisa wa magereza.
Rais JK na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe wakikagua mazao mbalimbali katika mabanda ya maonyesho.

Rais JK na Kamishna Jenerali John Minja wakiwa wamekaa kwenye kochi ndani ya banda moja la maonyesho. 
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto, Jerry Silaa akibadilishana mawazo na IGP Mangu.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete amelisifia Jeshi la Magereza kwa jitihada zao nzuri katika utendaji kazi pamoja na chagamoto nyingi walizonazo.

JK aliyasema hayo jana katika hafla ya Siku ya Magereza nchini ambapo sherehe hizo kitaifa zilifanyika kwenye Viwanja vya Chuo cha Maofisa Magereza kilichopo Ukonga jijini Dar es Salama na rais ndiye alikuwa mgeni rasmi.

Katika sherehe hizo, Rais JK aliwapandisha maofisa 104 ambao walikuwa wakifanya mafunzo kutoka cheo cha Inspekta na kuwa ASP ambapo kati ya hao 82 walikwa wanaume huku 22 wakiwa maofisa wa kike kati ya hayo 10 wakitoka Chuo cha Mafunzo, Zanzibar.

Rais aliahidi kushughulikia changamoto zinazolikabili jeshi hilo la magereza kabla hajaondoka madarakani na kumwagiza Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja kumwandikia barua Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani mahitaji yao yote ili aweze kuyashughulikia kabla ya kuondoka madarakani.

(PICHA ZOTE NA HARUNI SANCHAWA / GPL)

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini