Dotnata Aingilia Ugomvi wa WEMA SEPETU na KAJALA...Amuomba Mungu Haya Yatoke

!

Mwigizaji mkongwe, Husna Posh ‘Dotnata’ ameengilia kati ugomvi kati ya mastaa wa Bongo Movies, Wema Sepetu na Kajala Masanja kuwataka waachane na hali hiyo kwani bifu lao halina faida kwao na katika jamii.

Akizungumza na Tanuru la Filama hapo jana, Dotnata alisema kuwa kwa akili ya kibinadamu ugongvi huo hauwezi kuisha kutokana na kila mmoja kumuona mwenzake ndiyo mbaya.

Namuomba Mungu kila siku ili Wema amsamehe Kajala na Kajala amsamehe Wema ili maisha yaendelee kwani kwa akili za kibinadamu imeshindikana hivyo na nitaonana nao baada ya maombi yaha kwani natambua hakuna jamabo kubwa lisilo na mwisho, hasira zaozina mwisho” alisema Dotnata.

Dotnata pia alimtaka Wema ambaye ni sawa na mwanaye kuwa wa kwanza kumsamehe Kajala kwani kwenye ugomvi ni vizuri mmoja wapo ajishushe na kujona ni mkosaji kinyume na hapo hakuna ambacho kinaweza kufanyika.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini