HATIMAYE Mwili wa Mmiliki wa Shule Aliyeuawa Kinyama Jijini Dar Kisha Kutupwa Chooni Wapatikana!

Jeshi la Polisi Dar  limebaini mabaki ya mwili wa mmiliki wa shule ya Mtakatifu Zion, Anna Mizinga aliyeuawa Desemba mwaka jana na kutupwa kwenye shimo la choo cha shule yake.
Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es salaam Suleiman Kova alisema  mabaki ya mwili huo yalibainika Juni mwaka huu na tayari watu watatu wanashikiliwa na Polisi wakidaiwa kufanya unyama huo. 

Akifafanua juu ya tukio hilo Kova alisema  Februari mwaka huu mtu mmoja alitoa taarifa polisi juu ya kupotea kwa mmiliki huyo tangu Desemba mwaka jana saa 11 jioni na hakuonekana tena. 

Alisema mmiliki huyo alindoka nyumbani kwake na gari dogo aina ya Verosa akiwa na mtu mmoja ambaye naye ni miongoni mwa watuhumiwa wanaoshikiwa na jeshi hilo na abada ya taarifa hiyo walifungua jalada la uchunguzi na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao. 

Alisema mtuhumiwa wa kwanza alikamatwa Uchira, Moshi na kuwataja wenzake.
“Katika mahojiano mmoja alisema yeye na marehemu waliondoka hadi shuleni kwake na walipofika walivamiwa na watu wapatao wanne na kuanza kupigwa, lakini yeye alifanikiwa kutoroka na kujificha katika uzio wa shule, na aliwaona watu hao wakiendelea kumpiga mama huyo na kisha kumtupa katika shimo la choo kisha kutokomea na gari lake kusikojulika” Kova. 

Watuhumiwa hao wanaendele kuhojiwa ili kupata undani wa tukio hilo, ikiwa ni pamoja na kuwatafuta na kuwakamata watuhumiwa wengine wanaohusika na tukio hilo.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini