VIDEO: ALI KIBA katuonjesha kipisi cha sekunde 15 kutoka kwenye video yake mpya ya ‘cheketua’

Ali Kiba

Jumatatu ya June 29 2015 ndio itakua siku rasmi kwa video mpya ya ‘Chekecha’ ya Ali Kiba kuanza kuonekana kwenye TV ambapo TV ya kwanza kuplay hiyo video ni TRACE TV, TV ya burudani kutokea Ufaransa ambayo inaongoza kwa kutazamwa Afrika sasa hivi.

Tulianza kuzipata pichaz za behind the scenes toka South Africa ambako staa wa Bongo Fleva, Ali Kiba alikuwa anafanya video ya Chekecha Cheketua, baadae nikapita kwenye ukurasa wake Instagram na kukutana na uthibitisho kwamba Video hiyo itaoneshwa Exclusive kupitia #TraceTV… ninacho kingine kipya ha kushare na wewe!!

Wakati tukisubiria hiyo kesho kuitazama, kuna hizi sekunde 15 kazitanguliza Ali Kiba kutoka kwenye hiyo video.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini