Zoezi la kujiandikisha kwa mfumo wa BVR huko Morogoro Timbwili laibuka

Zoezi la uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura BVR katika manispaa ya Morogoro limezua tafrani katika baadhi ya katika kata ya kichangani manispaa ya Morogoro baada ya wananchi kusubiri muda mrefu bila kuandikishwa kufuatia ubovu wa mashine pamoja na kukosekana mpiga picha.

Mwandishi wetu ameshuhudia idadi kubwa ya wananchi waliopanga foleni wakisubiri kujiandikisha huku mashine zikionekana wazi bila mwandikishaji ambapo wananchi hao wametupia lawama tume ya taifa ya uchaguzi kushindwa kupeleka waandikishaji na badala yake hadi kufikia majira ya saa nane mchana hakuna mwananchi hata mmoja aliyeandikishwa huku wananchi wakiendelea kusota juani ambapo waomba tume ya uchaguzi kushughulikia haraka tatizo hilo ili wananchi wasikose haki yao ya kujiandikisha.
Wakati hayo yakijiri katika kituo hicho imezuka sintofahamu kati ya viongozi wa Chadema na CCM ambapo Chadema wakimtuhumu mwenyekiti wa mtaa wa Eria six kuwarubuni wananchi huku akiandika namba za simu zao pamoja na namba za nyumba wanazoishi jambo ambalo ni kinyume cha sheria za uandikishaji na hivyo kutaka mkurugezni wa manispaa ya Morogoro kutoa ufafanuzi juu ya uhalali wa viongozi wa serikali za mitaa kusimamia zoezi la uadikishaji. 
Awali mkuu wa mkoa wamorogoro Dokta Rajabu Rutengwe amezindua zoezi hilo kwa awamu ya pili katika manispaa ya Morogoro litakalohusisha kata saba ambapo amewataka wananchi wa Morogoro kuendelea kuwa wastahimilivu kwa matatizo madogo yanayojitokeza ili kila mwananchi aweze kutumia haki yao ya kidemokrasia kujiandikisha na hatimaye kuchagua viongozi waadilifu watakao liongoza taifa.

chanzo:itv habari

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini