Beyonce na Jay Z Wapigwa Bao na Taylor Swift na Calvin Harris kama ‘couple maarufu’ iliyoingiza fedha nyingi 2015

Taylor Swift na Calvin Harris wametajwa na Forbes kuwa couple maarufu iliyoingiza fedha nyingi zaidi mwaka 2015 na kuwaondoa Beyonce na Jay Z kwenye nafasi hiyo.
Swift na Harris wameingiza kwa pamoja dola milioni 146 mwaka jana ukilinganisha na Bey na Jay waliokamatana nafasi ya pili kwa kuingiza dola milioni 110.5.
Album ya Swift 1989 iliuza kuliko zote mwaka jana wakati Harris akiwa DJ anayelipwa zaidi duniani.
Swift pia ana endorsements kama za Diet Coke, Keds, na Sony.
Nafasi ya tatu imekamatwa na Blake Shelton na Miranda Lambert walioingiza dola milioni 57 mwaka jana.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini