MAAJABU! MAITI YAPUMUA WAKATI IKIOSHWA ILI IVISHWE SANDA, WAOMBOLEZAJI WATIMUA MBIO, MSIBA WAVUNJIKA!


Huko mjini Bagamoyo katika eneo lijukanalo kwa jina la Majani Mapana, mwanamama mmoja jana(juzi) aliyetambulika kwa jina moja la Bi. Hatujuani aliyethibitishwa kuwa umauti umekuta, alipumua wakati wakimkosha na kwa matayarisho ya kuvikwa sanda.

Bi. Hatujuani aliugua kwa muda na kukimbizwa hosptilai ya wilaya Bagamoyo na baadaye kudhaniwa kuwa ama amepatwa na umauti wa muda mfupi au kupoteza fahamu lakini hospitalini hapo walithibitisha kuwa keshakufa.

Mkasa huo ulitokea tarehe 28 Juni 2015 na wanandugu walishachukua maiti na matayarisho ya maziko yakiwa mbioni, turubai lilishafungwa,sanda tayari hadi Juni 29, 2015 wakimkosha maiti Bi. Hatu mwenye umri wa miaka 30, waliokuwa wakimkosha walishtuka maiti kuwa ana joto kali, anatoka jasho na anakunja na kukunjua mikono na miguu, lakini kusema wala kusimama hawezi!

Baada ya wanandugu kutangazia umma kuwa msiba hakuna tena bali tuna mgonjwa mahututi.
Waliofika msibani na umati wa watu waligoma kuondoka mazikoni hadi kieleweke nini kilichozua mtihani huu tena katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini