KUMBE Wizkid naye alifanya makusudi kutokwenda tuzo za BET, ameusema ukweli hapa..

wizkid

Toka tuzo za BET 2015 zifanyike juzi jumapili ya tarehe 28 June baadhi ya wasanii wakubwa kutoka Africa wamekuwa wakijitokeza kueleza sababu za kwanini hawakutokea kwenye tuzo hizo mwaka huu wakidai hawafurahishwi na kitendo cha TV hii kubwa ya burudani Marekani BET kuwatenga wasanii wa Kiafrika na wasanii wengine wakubwa wakati wa utoaji wa tuzo. 

Kwa sababu utaratibu ni kwamba Wasanii wa Afrika hupewa tuzo yao asubuhi wakati Wasanii wakubwa wa Marekani kama kina Beyonce na Chris Brown hupewa tuzo zao jioni kwenye tukio lenyewe huku wakishuhudiwa na wageni waalikwa, tofauti na wa Afrika ambao huwa hakuna mgeni hata mmoja kwenye ukumbi.
Hii picha ni wakati Davido wa Nigeria akipokea tuzo 2014, wanasema hata nyuso zao zilikua zinaonyesha hawana furaha kihivyo sababu waliitwa ukumbini asubuhi kabla ya tukio lenyewe jioni.
Hii picha ni wakati Davido wa Nigeria akipokea tuzo 2014, wanasema hata nyuso zao zilikua zinaonyesha hawana furaha kihivyo sababu waliitwa ukumbini asubuhi kabla ya tukio lenyewe jioni.
Jana msanii Fuse ODG ndio alitangaza kwamba hakwenda kwenye utoaji wa tuzo hizo sababu Wasanii wa Afrika wanadharaulika na kupewa tuzo backstage, saa kadhaa zilizopita aliefatia kwenye headlines ni Wizkid wa Nigeria anaesema hatokwenda kwenye hizi tuzo hizo kama BET wataendelea kuwapa wasanii wa Kiafrica tuzo zao nyuma ya pazia, yani Waafrika wanapewa tuzo saa nne asubuhi wakati kina Beyonce wanapewa jioni

Beyonce 
Yani yupo radhii awe anafanya shows tu kwa ajili ya mashabiki wake lakini sio kwenda kwenye tuzo za BET, huku akisisitiza kuwa anawapenda sana BET na anatambua mchango wao wa kuwainua wasanii wa kiafrika duniani na anajua sio rahisi kuandaa tukio kama hilo kila mwaka ila kwa style hii yupo radhii aende tu kama mtu mwengine wa kawaida kushuhudia tuzo.
Amesema ‘huwa sipost kuhusu kuchaguliwa kuwania tuzo na huwa siongelei pia kwasababu kiukweli sijali’
W1

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini