Safari ya LOWASSA Yaisha na Watu Zaidi Ya 800,000

Waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa amemaliza safari yake ya kusaka wadhamini katika Mikoa yote ya Tanzania na kujikusanyia zaidi ya wadhamini laki 8. 

Lowassa alianza safari ya kusaka wadhamini Juni 4 baada ya kuchukua fomu ya kugombea Urais kupitia CCM na jana amehitimisha safari yake hiyo katika Mkoa wa Morogoro. 

Hata hivyo kwa mujibu wa kanuni za CCM, kada anayewania kugombea Urais, anatakiwa kuwa na wanachama waliomdhamini 450 kutoka Mikoa 15 ikiwemo mitatu kutoka Zanzibar.

Katika baadhi ya Mikoa ambayo Lowassa alipata wadhamini wengi ni pamoja na Dar es salaam, Arusha, Morogoro, Pwani, Iringa, Mbeya, Ruvuma , Kilimanjaro, Tanga naSingida.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini