MCHEZAJI Aliyetoswa YANGA SC apewa miaka miwili SC Villa


Hans Mloli,Dar es Salaam

YULE kiungo Msierra Leone, Lansana Kamara aliyetoswa na Yanga kwa kushindwa kufuzu majaribio, hatimaye mambo yametiki baada ya benchi la ufundi la SC Villa kuikubali shughuli yake na kumjumuisha kundini kwa miaka miwili.
Kamara juzi aliichezea Villa katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Yanga kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, uliomalizika kwa suluhu.

Kocha Mkuu wa Villa, Kirya Ibrahim, ameliambia Championi Jumatatu kuwa ameridhishwa na kazi iliyoonyeshwa na Kamara katika mechi hiyo, hivyo atakwenda kuongea na uongozi wa timu hiyo wamsajili mchezaji huyo na anaamini atawasaidia kwenye timu yao.

“Ni mchezaji mzuri, nimemuona anafaa kwa jinsi alivyocheza leo (juzi), ana morali nzuri, anawajibika mapema na pia ana muunganiko mzuri, kitu kingine kizuri kwake ni kwamba anajua kupiga pasi nzuri na zinazofika, isipokuwa anahitaji kuwa fiti tu zaidi ya hapa, akishakuwa fiti atakuwa mzuri zaidi na msaada mkubwa lakini ukiniuliza kwa nini Yanga wamemuacha siwezi kukujibu, kila mtu ana maono yake,” alisema Kirya.
Katika mchezo huo na Yanga, Kamara alicheza kwa dakika 74 kabla ya kutoka na kumpisha nahodha wa timu hiyo, Isaac Kilwawila.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini