Alichoenda Kukifanya DIAMOND PLATINUMZ Huko Nigeria ni Hiki Hapa...

Ikiwa ni wiki chache zimepita toka aachie wimbo/video mpya ‘Nana’ , Diamond ametua jijini Lagos, Nigeria alikoenda kufanya promo zaidi ya wimbo huo aliomshirikisha msanii wa huko.

Diamond Platnumz akiwa ameongozana na team yake wakiwemo mameneja wake Salaam na Babu Tale, pamoja na Dj wake Romy Jons, ameenda nchini Nigeria kufanya media tour ya kuitangaza ngoma yake mpya aliyomshirikisha Flavour.
“Ofcourse am in Town already…. shukran sana #CocaCola kwa kuniwezesha kwenye safari hii ya kuja kuitandaza vyema #Bongoflavour yetu #LAGOS #IAmAreason Cc @romyjons @iam_kcee @salaam_sk”-alipost Diamond
Msanii Kcee wa Nigeria ambaye pia ametoa wimbo aliomshirikisha Diamond hivi karibuni ‘Love Boat’, ndiye ameonekana kuwa mwenyeji wao toka walipowasili uwanja wa ndege.
“Chilling with my peps @diamondplatnumz@babutale @romyjons @iamharrysong Live in Lagos” – alipost Kcee kwenye moja ya picha.
Siku chache zilizopita Diamond alifanya media tour nyingine Afrika Kusini kutangaza collabo mpya aliyofanya na msanii wa huko, Donald ambayo video yake pia imefanyika wiki iliyopita.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini