HALI NI MBAYA, NJAA ITATUUA -MTITU

MTITU42

Staa wa sinema za Kibongo, William Mtitu.
 Hamida Hassan
 Staa wa sinema za Kibongo, William Mtitu amefunguka kuwa, njaa itawaua mastaa wa tasnia hiyo kwa sababu mzunguko wa fedha umekuwa mgumu na hata kazi zao zinakwenda taratibu sokoni tofauti na miezi ya nyuma. 

Akipiga stori nasi, Mtitu alisema kuwa kwa sasa kila msanii utakayemuona atakwambia hana fedha kwani ni kipindi kigumu ambacho hakijawahi kuwatokea.
“Unajua kipindi hiki ni kigumu sana na hakijawahi kutokea ila siku si nyingi tuna imani mambo yatakuwa mazuri na tutarudi kama kawaida,” alisema Mtitu.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini