MASTAA WENYE SHOBO TZ WAMSHANGAZA TIKO WA BONGO MOVIES!

0f97tikoGladness Mallya

 STAA wa sinema za Kibongo, Tiko Hassan amewashangaa mastaa wenzake wanaowashobokea watangaza nia ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwani yeye kwa sasa hayupo upande wowote akisubiri atakayepitishwa ndipo aweke wazi mapenzi yake kwake. 

Akipiga stori nasi, Tiko alisema anawaonea huruma wasanii wenzake wanaodanganyika na fedha wanazopewa na watangaza nia hao ambapo baadaye wataona hasara na kujutia uamuzi wao kwani kiongozi anayefaa kwa jamii siyo yule anayetoa rushwa ili apitishwe. 

“Mpaka sasa siko kwa mgombea yeyote, nasubiri akishatangazwa mmoja na chama ndiye nitakayemsapoti, nawashangaa na nawaonea huruma sana wanaodanganyika na mishiko ya wagombea kwani itawagharimu na vizazi vyao vijavyo,” alisema Tiko.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini