MWIGULU NCHEMBA Aibuka Kidedea Mbio za URAIS 2015

Taasisi ya Utafiti wa Maendeleo ya Elimu Tanzania (TEDRO) imetoa matokeo ya utafiti kuhusu wagombea ambao hotuba zao ziligusa mahitaji wa wananchi kuwa Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba ndiye aliyeibuka kidedea.

Mkurugenzi wa TEDRO, Jacob Kateri alisema lengo la utafiti huo ilikuwa kujua ni kwa kiasi gani Watanzania wanafuatilia mchakato mzima wa kuelekea uchaguzi mkuu, hususani kipindi hiki cha watu kutangaza nia na kutambua mchango wa vyombo vya habari kufikisha elimu ya uraia kwa umma tunapoelekea uchaguzi mkuu.

Alisema utafiti huo umefanywa katika za Njombe Mjini na Vijijini, Mbeya Mjini, Rombo, Arumeru, Kinondoni, Kilombero na Kibaha vijijini. Wakati wilaya walizohojiwa kwa simu ni zingine zilizosalia kwa kuzingatia kwamba kumbukumbu za wahojiwa za simu zinapatikana katika ofisi yetu.

Mkurugenzi huyo alisema uchambuzi wa kujua nani anayewafaa wananchi kupitia vipaumbele vilivyoainishwa na watangaza nia, kutathmini hotuba iliyo bora kwa kuzingatia yaliyomo na mahitaji ya Watanzania na nini yaweza kuwa agenda ya msingi tunapotarajia kumpata Rais wa awamu ya tano. 

Alisema katika sehemu ya uadilifu usiotiliwa shaka, matokeo yanaonesha kuwa Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba anaongoza kwa kupata asilimia 15. Aliyefuata ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe 13 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Kazi Maalumu, Mark Mwandosya 13.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda asilimia nane, Naibu Waziri Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba nane, Jaji Mkuu Mstaafu, Augustino Ramadhani saba, Waziri Mkuu wa aliyejiuzulu, Edward Lowasa 10, Makongoro Nyerere tano na waliosema hakuna msafi ni wananchi 12.

Pia kuhusu kipengele cha hotuba bora Mwigulu aliongoza kwa kupata alama A, akifuatiwa na Januari, Wasira, Profesa Mwandosya, Profesa Muhongo , Wasira na Membe walifungana kwa kupata alama B+, Lowasa, Mbunge wa Sengerena William Ngeleja walifungana kwa kupata alaba B.

“Tathmini ya hotuba imezingatia utulivu katika uwasilishaji, mkusanyiko wa mambo yanayohusu wananchi wa makundi yote ya jamii katika hotuba, uwezo wa kujibu maswali na ufafanuzi wa mambo mtambuka ya kiuchumi ikiwamo kushuka kwa thamani ya shilingi, na njia za utatuzi kwa nchi kama Tanzania,” alisema.

Kuhusu kipengele cha mtangaza nia wenye uwezo wa kupambana na vita ya rushwa na kuboresha utawala bora, matokeo yalionesha kuwa Mwigulu anaongoza asilimia 17, Dk Magufuli 14, Membe 11, Lowasa 6.10, Jaji Ramadhani sita.

Profesa Mwandosya, Pinda na Mwakyembe walifungana kwa kupata asilimia nane, Januari saba, Waziri wa Uchukuzi Samuel Sitta sita, Kigwangala tatu, na wengine nne.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini