Lowassa Awaburuza Wenzake Urais CCM...... Ni matokeo ya utafiti kwenye wilaya 20

Waziri Mkuu mstaafu, Monduli, Edward Lowassa ametajwa kuongoza katika kutaja vipaumbele vya maendeleo ikiwamo kupunguza tatizo la Ajira nchini na kuinua Elimu, miongoni mwa kundi la wanasiasa waliotangaza nia ya kuwania Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

 Kadhalika, Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, ametajwa kuwa ndiye kiongozi wa siasa aliyeshuhudiwa na wananchi wengi katika hotuba zake kuliko wanasiasa wengine waliokwisha kutangaza nia.

Hayo yamo katika ripoti ya utafiti uliofanywa na Shirika la Maendeleo la Utafiti la Elimu (Tedro), iliyozinduliwa jijini Dar es Salaam jana.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Jacob Katerri, alisema ripoti hiyo ilijumuisha Wilaya 20 na kuwahoji watu 2,000 kutoka vijijini na mijini.

 Alisema katika ripoti hiyo kipengele cha watangaza nia walioshuhudiwa na watu wengi katika hotuba, Lowassa anaongoza kwa kushuhudiwa kwa asilimia 54, akifuatiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (46), Naibu Waziri wa Fedha ,  Mwigulu Nchemba (44), Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Steven Wasira (40) na Jaji Mkuu mstaafu Augustino Ramadhani(39).

 Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, January Makamba(34), Waziri Nchi Ofisi ya Rais, Profesa Mark Mwandosya (31), Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki,  Makongoro Nyerere (27), Waziri wa Ujenzi, John Magufuli (23), na Mbunge wa Sengerema, Willium Ngeleja (19) na wengine wakifuata.


Katika Kipengele cha kupunguza tatizo la ajira, ripoti hiyo ilieleza kuwa wananchi walipohojiwa walieleza kuwa wana imani na Lowassa kwa asilimia 19,  Nchemba (14), Magufuli (13).

 Makamba (13), Membe (12), Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (10), Mwandosya (7), Dk. Harrison Mwakyembe (7), Wassira (2) na wengine (3).

“Utafiti huu umebaini kuwa watangaza nia wengi pamoja na mambo mengine walijikita sana katika kusema watatatua tatizo la ajira kwa vijana,” alisema  Kaserri.

Kadhalika ripoti hiyo ilizungumzia kipengele cha kuinua elimu nchini, ambacho wananchi waliohojiwa walitoa nafasi kubwa ya uwezekano wa kutekelezewa kwa kipaumbele hiki kwa Lowassa kwa asilimia 25.

Nchemba (18), Membe (16),  Makamba (13), Magufuli (12), Mizengo Pinda (12), Wasira (3) na wengine (9).

 Pia ripoti hiyo ilizungumzia kipengele cha Tanzania kuwa nchi ya kipato cha kati ifikapo waka 2025, na wananchi walikuwa na imani na Nchemba kwa asilimia 13.4 kuwa ataweza kulipeleka taifa kufikia kipato cha kati.

Lowassa (11), Wasira (9), Membe (9.20),   Magufuli (9.0), Makamba (5.3), Mwandosya (4.60),  Pinda (3.5) na Dk.  Mwakyembe (1.40).

Hata hivyo, utafiti huo ulielezea kipengele cha kuinua sekta ya Kilimo na Mifugo nchini ambacho kwa watangaza nia hao, wananchi walikuwa na imani kwa Pinda kwa asilimia 23.

Lowassa (17), Nchemba (16), Membe (11) Wasira (9),  Makamba (7), Magufuli (5), Waziri wa Maliasili na Utalii,  Lazaro Nyalandu (3.3), Mbunge wa Nzega, Hamisi Kigwangala(3.2) na Mwakyembe (2.6).

Katerri alisema utafiti huo pia ulihusu kipengele cha Utawala bora na vita dhidi ya ufisadi ambapo ulionyesha kuwa Mwigulu Nchemba amepata asilimia 17.4 ya uwezo wa kupambana na tatizo hilo.

Wengine waliomfuata ni Magufuli (14.2), Membe (11), Lowassa (6.10), Jaji Ramadhani (6) na Mwandosya (5).

Wengine ni Mizengo Pinda (8),  Mwakyembe (8),  Makamba (7), Samuel Sitta (6), Dk. Kigwangala (3).

Katika kipengele za Uadilifu usiotiliwa shaka katika utumishi Nchemba alipata asilimia 15, Membe (13), Mwandosya (13), Pinda (8), Makamba (8) Jaji Ramadhani (7),  Lowassa (10%).

Katika kipengele cha hotuba iliyo bora, Katerri alisema Nchemba alipata alama (A), Wasira( B+), Membe (B+),  Mwandosya (B+) Lowassa (B) na Membe (B). Katerri Alisema lengo la utafiti huo ni  kutathmini Elimu katika Nyanja ya uraia kwa watanzania kupitia vipaumbele katika hotuba za waliokwisha kutangaza nia kupitia CCM.

Alizitaja wilaya ambako utafiti huo ulifanyika kuwa ni  Kinondoni, Kibaha Vijijini, Kilombero, Rombo, Arumeru, Mbulu na Babati, Lindi, Mtwara, Njombe mjini, Njombe Vijijini, Mbeya Mjini, Nyamagana, Biharamulo, Tabora, Nzega, Bahi, Chamwino na Kasulu.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini