Maneno mengine ya Ommy Dimpoz kuhusu waliomtukana Instagram…UHearD (Audio)

Ommy Dimpoz alipost tangazo la Video mpya ya Ali Kiba lakini baada ya kupost wapo waliopita kwenye post yake @Instagram na kuanza kuandika comments za matusi.

Mwenyewe amesema hakupenda kuona watu wanaandika comments za matusi kila kitu ambacho anapost… Ommy amesema kwenye kurasa za mastaa kama yeye wanaopita ni watu wengi kwa hiyo sio kitu kizuri watu kuandika lugha za matusi.

Mitandao huwa inakuwa na story nyingi sana kuhusu mastaa, wakati mwingine utasikia staa fulani na fulani hawapatani, Ommy amesema wakati mwingine watu huwa wanakuza hata beef kati ya mastaa lakini beef nyingine sio za kweli.
Nimekuwekea sauti waweza sikiliza live hapa chini...

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini