HUKUMU YA MRAMBA, YONA NA MGONJA...HAYA NDIO MAAMUZI YALIYOCHUKULIWA NA MAHAKAMA HIVI PUNDE!

HUKUMU ya aliyekuwa Waziri wa Fedha, Basir Mramba, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Gray Mgonja na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona imeahirishwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam hadi Julai 3, mwaka huu!   

 Vigogo hao wanakabiliwa na mashtaka ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya Shilingi bilioni 11.7
Kesi hiyo imeahirishwa baada ya kutokuwepo Hakimu Saul Kinemela ambaye ni mmoja wa jopo la mahakimu watatu wanaosikiliza kesi hiyo. Mahakimu wengine wanaoongoza jopo hilo ni Jaji John Utamwa na Jaji Sam Rumanyika. 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jaji John Utamwa leo ni kwamba Hakimu Kinemela yupo mkoani Dodoma kwa shughuli maalum za kibunge na anatarajia kurejea jijini Dar kati ya kesho au keshokutwa, hivyo hawawezi kutoa hukumu hiyo bila jopo hilo kukamilika.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini