MAJONZI TELE: DAMU YATAPAKAA WAKATI MOTO UKIJERUHI WATU 500 HUKO TAIWAN LEO-PICHAZ

 

Majeruhi katika ajali hiyo wakipatiwa huduma ya kwanza.
WATU zaidi ya 500 wamejeruhiwa kufuatia kutokea mlipuko na moto kwenye bustani moja ya burudani nchini Taiwan mapema leo.

Rais wa Taiwan, Ma Ying-jeou (katikati) akiongea na mmoja wa majeruhi aliyelazwa hospitalini baada ya ajali hiyo.
Watu takribani 200 wamejeruhiwa vibaya kwenye ajali hiyo iliyotokea karibu na Mji Mkuu wa Taipei wakati kitu kisichojulikana kinachofanana na unga kilipolipuka kwenda hewani.

Damu zikiwa zimetapakaa eneo la ajali hiyo.
Baadhi ya watu wanaaminika kupumua unga huo hali iliyosababisha wapate matatizo katika mifumo ya upumuaji.

Moto ukiwaka eneo hilo.
Picha za video zilionyesha watu wakilia huku waokoaji wakiwabeba wale waliopata majeraha ya moto huo.
Uchunguzi wa kubaini kilichosababisha moto huo unaendelea.
Zifuatazo ni picha zaidi za tukio hilo. 

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini