Walimu wanyolewa Nywele sehemu za siri kishirikina

WALIMU katika shule ya msingi  Nambaza Kata ya Nansimo wilayani Bunda,    wamesema watahama shule hiyo endapo serikali ya wilaya hiyo haitachukua hatua madhubuti kukomesha ushirikina shuleni hapo.

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Sospiter Mafuru,  alisema walimu wake wanafanyiwa vitendo vya ushirikina ikiwa  ni pamoja na kusumbuliwa   usiku  na kunyolewa  nywele   sehemu za siri.

Alitaja vitendo vingine kuwa ni kuvuruga vyombo vya ndani wakati wa usiku, kumwaga michuzi na damu kwenye mashuka na nguo za walimu hao.

“ Vitendo hivi vimetishia usalama wa walimu hadi sasa walimu watatu wa kike wamehama shule hii kwa hiyo tunaomba jamii ya Nambaza wachukue hatua,”alisema.

Alisema awali   ushirikiana huo ulianza kwa wanafunzi  kuugua na kuanguka ovyo na baadaye kwa walimu na aliomba Serikali   kuchukua hatua na kukaa na wananchi wao.

Mafuru alisema hadi sasa ana    walimu tisa,wa kike watano na wa kiume wanne.

 Mkuu wa wilaya ya Bunda, Joshua Mirumbe, alisema  tayari ameviagiza vyombo vya dola kwenda kijijini hapo kufanya utafiti kuwabaini watuhumiwa hao.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini