PICHAZ: Steve NYERERE Atikisa Jimbo la Kinondoni

Staa wa Bongo Movies, Steven Mangere ‘Nyerere’ amewaomba wanawake wasihadaike na kanga na vitenge wakipewa na baadhi ya wagombea wa nafasi mbalimbali za uongoziili wawachague.

Steve aliitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam, alipokuwa akitangaza nia yake ya kugombea ubunge jimbo la Kinondoni kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM) nakuwahimiza vijana wa Kinondoni wajitokeze kujiandikisha kwenye daftari la kudumu ili waweze kuchagua viongozi watakaoweza kuifikisha Kinondoni sehemu wanayotaka.

Katika mkutano huo, Steve alisindikizwa na wasanii mbalimbali akiwemo JB, Wasta, Bi Mwenda, Chuchu Hans, Johari,Ray Nyamayao, Esha Buheti, Thea na Bi Star

“Kinondoni tunaweza kuondokana na mafuriko kama tutachagua kiongozi atakayeweza kurekebisha miundombinu ya wilaya yetu”alieleza Steve huku akishangiliwa.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini