MWALIMU Mstaafu Aliyembaka Mjukuu Wake Huko Mpanda, Katavi Atupwa Jela Maisha!

Mahakama ya Wilaya ya Mpanda, Katavi imemuhukumu mwalimu mstaafu wa shule ya msingi  Mpanda Ndogo , Rashid  Ndogo mwenye miaka 65 kifungo cha maisha jela baada ya kumbala mjuu wake wa miaka mitano na kumuharibu vibaya sehemu zake za siri.

Hukumu hiyo ilitolewa jana na hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda, Chiganga Ntengwa baada ya mahakama kuridhika na ushahidi uliotolewa na pande zote mbili za mashtaka na utetezi. 

Awali katika kesi hiyo mwendesha mashtaka alidai mahakamani kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Oktoba mwaka jana majira ya saa 2 na nusu usiku nyumbani kwake katika kijiji cha Majalila.

Siku hiyo mshatakiwa alidaiwa kumbaka mjuu wake wakati amelala chumbani akiwa na mtoto wa mshtakiwa ambaye alishugudia baba yake akitenda kosa hilo la kinyama. 

Siku ya tukio mke wa mshatakiwa alimwaga mume wake kuwa amekwenda kufunga zizi la mbuzi lililokuwa jirani na nyumbani kwao na mumewe kutumia mwanya huo kuingia chumbani kwa mjuu wake na kuanza kumbaka huku mwanaye akishuhudia.

Mshakiwa alikamatwa na majirani siku hiyo na kupelekwa kituo cha Polisi ambapo alifunguliwa mashtaka huku mjukuu wake akikimbizwa hospitali kupatiwa matibabu.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini