HABARI NJEMA: Director Justin Campos wa S.A aja kushoot video Tanzania na kumchagua Hanscana kuwa mwenyeji wake (PICHAZ)

Director aliyefanya video za Vanessa Mdee ‘No Body But Me’ na ‘Nusu Nusu’ ya Joh Makini, Justin Campos wa kampuni ya Gorilla Films ya Afrika Kusini alikuja Tanzania kushoot video ya msanii wa Ghana wiki hii.


Hansana na Campos-1Hanscana, Justin Campos na Khalfani wakiwa location

Ma-director wa Tanzania, mshindi wa Tuzo Za Watu 2015 Hanscana na rafiki yake wa karibu Khalfani ndio walichaguliwa na director huyo kuwa wenyeji wake waliomsaidia kuanzia kutafuta vifaa hadi kwenda location Zanzibar. 

Hanscana ameiambia Bongo5 kuwa ukaribu wake na Campos umetokana na connection aliyopewa na Vanessa.

“Kina Vanessa kipindi anaenda kufanya kazi (Afrika Kusini) alikuwa anamuonesha video zilizopita ndio Justin akaona video za Hansacana kama mara mbili mara tatu, akauliza huyu Hanscana ni nani? Akaambiwa ni director wa Tanzania. Tukajuana tukawa marafiki kuchat Whatsapp hivyo yaani, tuna mipango mingi kufanya mabadilishano ya kibiashara.”

Hansana na Campos-2

Ameongeza kuwa Justin alimpigia na kumwambia kuwa anakuja kufanya video Zanzibar na kuhitaji awe mwenyeji wake pamoja na kumtafutia baadhi ya vifaa.

“Tulimsaidia kumpelekea vifaa si unajua bongo hapa hawezi kujua wapi atapata vifaa, vifaa vyote katumia vya hapa kasoro Camera ndo alikuja nayo.” Alimaliza.

Video zingine zilizofanywa na Justin Campos ni pamoja na video mpya ya Sarkodie ft. Ace Hood ‘NewGuy’, ya RunTown ft. Uhuru ‘The Banger’ pamoja na video ya Yemi Alade ‘Taking Over Me’.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini