BUSUNGU wa YANGA SC na KUFURU ya Mabao VPL

busu2Straika mpya wa Yanga, Malimi Busungu.

Saphyna Mlawa!  
Dar es Salaam
UNAWEZA ukadhani ni utani lakini ndivyo alivyotamka straika mpya wa Yanga, Malimi Busungu kwamba msimu ujao wa Ligi Kuu Bara atahakikisha anafanya kufuru ya kufunga mabao katika ligi hiyo kwa kufunga mabao 30.

Busungu aliyejiunga na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Mgambo JKT, alimaliza msimu uliopita akiwa na mabao tisa huku kinara akiwa Simon Msuva aliyefunga mabao 17.
IMG_201506175_121423 

Katika miaka ya hivi karibuni kwenye historia ya ligi hiyo, aliyekuwa straika wa Mtibwa Sugar, Abdallah Juma alifanikiwa kufikisha mabao 25, mwaka 2006, ambayo ni mengi huku rekodi yake ikiwa imedumu mpaka leo.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Busungu alisema kwa kushirikiana na wenzake atahakikisha anajituma kufikia malengo yake huku akiwamwagia sifa makocha wake, Hans van Der Pluijm pamoja na msaidizi wake Charles Boniface Mkwasa kutokana na ufundishaji wao wa kueleweka.

“Nimepanga kuhakikisha msimu ujao nafikisha mabao 30 na kuibuka kinara wa kuzifumania nyavu, kila kitu kinawezekana na kama ukiweka malengo halafu ukashirikiana vizuri na wenzako bila shaka utafanikiwa, ndivyo mimi nitakavyofanya msimu ujao,” alisema Busungu ambaye tayari ameshaanza kuonyesha cheche zake katika muda mfupi tu tangu atue Yanga.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini