MTUKUTU Kim Kadarshian kwenye headlines, azungumzia mpango wa kurudi shule!!

kk

Kim Kardashian ni mwanadada ambaye anajulikana kwa kutengeneza headlines nyingi sana na moja kati ya headlines anazoziweka public personality huyu ni zile zinazohusu uzuri wake. Lakini Kim anasema amechoshwa na fikra za watu wengi wanaodhani kuwa yeye ni mwanamke mzuri tuu asiye na akili ya kufikria mbali, na kwa sababu hiyo staa huyu ameweka headlines nyingine kubwa, ametangaza kurudi shule! 

Kim Kadarshian amesema anahisi yeye kama mtu binafsi hana uwezo mkubwa wa kutosha kiakili. Licha ya mamillioni na umaarufu wote alionao sasa hivi, Kim ameamua kurudi shule kupanua IQ huku akidai IQ yake haiko kwenye levo anayoitaka na anaona bora arudi kusoma, ameshapata umaarufu na pesa yupo tayari kuwekeza nguvu zake kwenye vitu vingine anavyoona ni muhimu na mume wake Kanye West amekua akimsisitiza Kimkujaribu vitu tofauti haswa kipindi hiki ambacho ana mimba. 
Lakini kumekuwa na baadhi ya watu wanaohisi kuwa jambo hili sio la ukweli na Kim anataka kupata watazamaji wengi zaidi wa Tv reality show yake Keeping up with The Kadarshians lakini msemaji wa Kim amepinga maneno haya na kusema kuwa staa huyo yupo serious na kurudi kusoma, na yeye kupata watazamaji wengi zaidi haiusiani ya maamuzi yake binafsi. Kwenye interview aliofanya, staa huyo alisema; 

>>> “Nahisi nishafanikisha lengo la kuwa maarufu na tajiri, kwa kipindi cha zaidi ya miaka kumi na kitu hilo ndio lilikua lengo langu, likatimia, nikajulikana, nikawa tajiri, nikaolewa na kuzaa mtoto wangu wa kwanza na sasa nategemea mtoto wa pili, nahisi umefika wakati wa mimi kurudi kusoma”. >>> Kim Kadarshian. 

Msemaji mkuu wa Kim Kadarshian amesema kwa sasa wanaangalia namna ya kufanikisha zoezi la yeye kupata vipindi maalum nyumbani kwake kwa ushirikiano wa mwalimu atakayekuwa tayari kumsaidia kufanikisha lengo hili.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini