GOOD NEWS: Nyota Ya YAMOTO Band Yazidi Kung'ara..Hiki Hapa Kitu Kipya Toka Kwao!

Nyota za vijana wa Yamoto Band inaendelea kung’ara, baada ya kushoot video na Godfather Afrika Kusini wiki chache zilizopita, vijana hao wamepata mwaliko wa kwenda kuwaburudisha Watanzania na wana Afrika mashariki waishio Marekani.

Mkubwa Fella ameiambia Bongo5 kuwa mwaliko huo wameupata siku chache zilizopita kutoka kwa Watanzania waishio huko.
“Mpaka sasa hivi watafanya show miji miwili lakini Minnesota nao wametaka halafu na New Jersey kuna Watanzania wanaoishi kule nao wamehitaji, lakini mpaka sasa hivi waliotuletea mikataba ni sehemu mbili ila kuanzia jana watu wengi nao wametaka madogo waende.”Alisema Fella. 

Show ya kwanza itafanyika Novemba 28, 2015 huko Houston Texas, ikifatiwa na show ya pili Desemba 5, 2015- Washington DC.
Mmoja wa mapromota wa Marekani alipost kuhusu ziara ya Yamoto band Marekani: yamoto usa
Mwaka 2015 umekuwa na mafanikio kwa Yamoto kimataifa, miezi michache iliyopita waimbaji hao wa ‘Ntakupwelepweta’ walitumbuiza nchini Uingereza pamoja na Muscat.
Fella ameongeza kuwa Video mpya walioyoshoot Afrika Kusini itatoka baada ya Ramadhan.
-via bongo5

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini