MWANAMUZIKI Diamond Platnumz Ashikiliwa Airport kwa Saa Mbili Kisa Madawa ya Kulevya..

Musa Mateja

KIBANO! Staa wa Bongo Fleva mwenye jina kubwa Afrika, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, juzikati alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya ‘kutaitiwa’ kwa saa mbili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kisa kikiwa wingi wa mabegi (3) makubwa aliyoshuka nayo akitokea nchini Afrika Kusini ‘Sauzi’, Ijumaa Wikienda linakupa ‘unyunyuz’ kamili.


Tukio hilo lililoshuhudiwa hatua kwa hatua na gazeti hili, lilijiri Juni 26, mwaka huu kwenye eneo la kukagulia mizigo ya abiria uwanjani hapo kitendo kilichosababisha Diamond kutokwa na kijasho chembamba.


TAFSIRI YA MABEGI MAKUBWA

Chanzo chetu kilichokuwa ndani ya jengo la kutokea abiria kililiambia Ijumaa Wikienda kuwa, maafisa ukaguzi wa uwanja huo walimtilia shaka Diamond hivyo ikawalazimu wayakague mabegi hayo hadi ndani lakini pia walimkuta ana upungufu wa stakabadhi za mizigo hiyo.

KUHUSU STAKABADHI

Kuhusu stakabadhi zisizokuwepo, ilibidi Diamond ampigie simu ‘mdogo wake’ (si wa tumbo moja) aliyejulikana kwa jina la Q-Boy ampelekee kwani alitua nazo Bongo siku moja kabla, yaani Juni 25.

NDANI YA MABEGI

Ndani ya mabegi hayo, kulikutwa kamera, maiki na vifaa vya studio.

IMANI YA WAPEKUAJI

Shuhuda mmoja ambaye Ijumaa Wikienda lilimkuta nje ya chumba ambacho Diamond alikuwa akipekuliwa, alisema maafisa hao waliamini msanii huyo alikuwa ameshuka na madawa ya kulevya ‘unga’.“Unajua mastaa siku hizi wanaongoza kwa kubeba unga. Sasa serikali iko makini nao sana. Ndiyo maana wengi wao wakipita hapa wanakaguliwa kuliko abiria wengine,” alisema mtu huyo aliyejitambulisha kuwa ni dereva wa teksi uwanjani hapo.

DIAMOND APIGWA PICHA, AONGEA NA WIKIENDA

Paparazi wetu aliendelea kuganda mlangoni hapo hadi Diamond alipotoka na kumfotoa picha mbalimbali na baadaye alimfuata hadi kwenye gari aina ya Toyota Lexus na kumuuliza kama anajua kisa cha kupekuliwa kwa muda mrefu vile.

“Nilikuwa na mizigo naishughulikia ili itoke hivyo kuna mambo pia tulikuwa tunapishanapishana pale maana walihitaji nilipie ushuru wakati vifaa vya studio tulishaambiwa ni ‘free’ (bure). Pia kulikuwa na risiti za mizigo ambazo zilikuwa hazionekani, kumbe Q-Boy alitangulia nazo jana mimi nikawa nimesahau.

“Ila wao walikuwa wakijiridhisha kwenye mizigo yangu. Walifikiri nimebeba unga,” alisema Diamond.

HALI YA SASA UWANJANI

Mbali na Diamond kupekuliwa kwa muda mrefu, kwa sasa abiria wanaoingia na kutoka kwenye uwanja huo wamekuwa wakikaguliwa kwa umakini ili kubaini uhalali wa mizigo yao lengo kubwa ni kudhibiti uingiaji au utokaji wa madawa ya kulevya ambapo serikali imeweka umakini katika kupambana na biashara hiyo haramu.

CHRISTIAN BELLA

Ukiachana na Diamond, mastaa wengine waliowahi kukumbana na pekuapekua kama hiyo ni Mkurugenzi wa Bendi ya Malaika, Christian Bella na mtangazaji wa Radio Time FM, Hadija Shaibu ‘Dida’.

Bella yeye alikumbwa na adha hiyo, mwaka juzi, usiku wa saa nane akiwa anatokea nchini Uturuki na Ndege ya Shirika la Turkish Airways.

Dida naye ilikuwa mwaka 2012 ambapo alikumbwa na pekuapekua hiyo alipoingia uwanjani hapo kuelekea nchini Thailand kwa shughuli za kibiashara.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini