LAZIMA UKAE! Maneno ya utani ya Rais Mugabe kwa Obama baada ya kuruhusu ndoa ya jinsia moja…

 

Ndani ya wiki moja baada ya Serikali ya Marekani kupitisha Sheria ya kuruhusu Ndoa za jinsia moja kwa raia wake kumekuwepo na maoni mbalimbali kutoka kwa watu kuhusiana na maamuzi hayo.

Mmoja wa watu walioguswa na maamuzi hayo ni Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe ambaye ameeleza hisia zake baada ya maamuzi hayo kupitishwa.

Rais wa Marekani Barack Obama 
Katika mahojiano na radio ya Taifa ya Zimbwabwe, Mugabe alisema hawezi kupingana na maamuzi ya nchi hiyo kwani ni sheria ambayo imepitishwa na Serikali na kama ni hivyo ataamua kufunga safari kwenda mpaka Washington kuomba kufunga ndoa na Rais Barack Obama.

Ameongeza kuwa, Serikali ya Marekani imekuwa ikiongozwa na wajinga ambao ni wafuasi wa shetani wanaoitukana taifa la Marekani akisisitiza Marekani imechafuka na wanaiendesha nchi kwa dhana zao binafsi ambazo ni potofu.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini