AIBU KUBWA! (A LOOKBACK)

Stori: Chande Abdallah na Denis Mtima, Mwanza
NI aibu kubwa! Mpigachabo maarufu nchini, Andrea Masangu (29) amenaswa akiwa kwenye uvungu wa kitanda akiwapiga chabo wanandoa, Ijumaa Wikienda lina mkasa wote mkononi.


 Mpiga chabo akitolewa uvunguni baada ya kunaswa.
Tukio hilo lilitokea Januari 10, mwaka huu, ndani ya Gesti ya Riverside, Stendi ya Nyegezi jijini hapa ambapo kijana huyo aliingia kwa kuruhusiwa na mhudumu wa gesti hiyo katika mtego makini uliotegwa na Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers na mwishowe kujikuta akiumbuka.
OFM WAPOKEA MASHTAKA
Wiki moja nyuma, mtu mmoja alipiga simu kwa OFM jijini Dar akidai yeye ni msomaji wa Magazeti Pendwa ya Global. Akasema ameamua kupiga simu ili kumshtakia Andrea akidai amekuwa na tabia iliyoota sugu ya kupiga chabo wapenzi wanapokuwa gesti.
“Mimi naitwa…(akataja jina lake), napiga simu kutoka jijini Mwanza. Kuna bwana mmoja anaitwa Andrea, amekuwa na tabia ya kuwachungulia (kuwapiga chabo) wapendanao wanapokuwa gesti.
“Mbaya zaidi, huyu jamaa nasikia huu mtindo anao siku nyingi sana. Amekuwa akienda hata nje ya Mkoa wa Mwanza kwa ajili hiyo,” alisema mtoa habari huyo.
Akaongeza: “Kuna watu wanasema kuwa hata Tabora, Dodoma wanamjua kwa tabia hiyo. Hebu OFM njooni Mwanza.
Ijumaa Wikienda: Usipate tabu, hukohuko Mwanza kuna OFM wametokea hapa makao makuu. Nawapa namba yako ili mshirikiane.
Mtoa Habari: Mtakuwa mmefanya jambo la maana sana.

Mpiga chabo baada ya kutolewa uvunguni.
KAZI YAANZA
Ndani ya dakika tano tu, OFM waliopo Mwanza wakapewa namba za mnyetishaji wetu, kazi ikaanza.
OFM Mwanza, walimtafuta mtoa habari huyo na kukaa naye meza moja ambapo walipanga mipango.
Miongoni mwa mipango hiyo ilikuwa ni pamoja na kutoa taarifa kwenye kituo cha polisi jijini Mwanza ambapo maafande walijipanga.
SIKU YA TUKIO
Siku ya tukio, Andrea alikwenda kwenye gesti hiyo na kumuuliza mhudumu kama kuna wateja wa ‘shot’ taimu’ wataingia, akajibiwa wapo njiani.
Akaomba alipe shilingi elfu mbili (2,000) ili atangulie kuingia yeye kwenye chumba ambacho mhudumu huyo atahakikisha anawaingiza wapendanao hao.
OFM WAJULISHWA, WAINGIA
OFM walijulishwa kuwa mpiga chabo huyo amewasili na tayari ameingia chini ya kitanda kwenye gesti
hiyo, nao wakamchukua OFM mwanamke na kutinga naye sanjari na Polisi wa Dawati la Jinsia Jiji la Mwanza.

OFM WAMCHEZEA MCHEZO
Ndani ya chumba hicho, wapendanao (mke na mume) hao walifikia kitandani. Lakini ili kujiridhisha kama kweli Andrea alikuwa uvunguni, OFM mwanaume alijifanya ameangusha pesa chini, alipoinama kuiokota akamuona kiaina lakini hakuonesha kushtuka.
Ndipo OFM hao ‘wapendanao’ walianza kuchojoa nguo za juu na kuzitupa chini kana kwamba walikuwa tayari ‘mchezoni’ ili kumshawishi Andrea aendelee kuamini na kufurahia dhamira yake chafu.
OFM NJE YA GESTI
Nini kilibaki hapo kama si OFM waliokuwa chumbani kuwajulisha kwa simu wenzao waliokuwa nje na polisi?
Chumba kilivamiwa, Andrea akajikuta yuko chini ya mikono ya sheria akionekana ameingilia faragha.
ETI AKAJITETEA!
Baada ya kutolewa chini ya kitanda, Andrea aliwekwa mtu kati na kuhojiwa kulikoni kuwa mpiga chabo wa kiwango kile?
Andrea alianza kwa kuomba msamaha na kuahidi kuacha kabisa tabia hiyo. Alikiri amekuwa akichungulia watu wengi sana wanaofika katika gesti za jijini Mwanza.
“Jamani nimekoma, ni shetani tu, naacha kabisa mambo haya ‘haki  ya Mungu’ kuanzia leo sifanyi tena.
“Kweli nimewachungulia watu wengi sana na sijapata faida yoyote, sijui shetani gani aliniingia,” alilalama Andrea na kuongeza kuwa hayupo peke yake bali ana marafiki zake wengi ambao hufanya kama anavyofanya yeye.
Soo hilo liliisha kwa Mshauri Nasaha wa Taasisi ya Farijika, Aisha Mtumwa kumrekebisha kisaikolojia Andrea sambamba na kumpa onyo kwamba akirudia tena atatupwa rumande kwa kosa la kuingilia faragha ya watu.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini