SUMATRA YAZIFUNGIA DALADALA ZA KIMARA KARIAKOO KISA SHILINGI 800
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu
na Majini (Sumatra) imeifungia daladala zinazofanya safari zake Kimara
hadi Kariakoo kwa siku 30 kutokana na kuwatoza abiria nauli ya Sh. 800
tofauti na iliyopangwa na mamlaka hiyo.
Kwa
mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi Mkuu wa Sumatra, Michael Kisaka alisema
wameamua kuwafungia na endapo watakiuka masharti hayo watachukuliwa
hatua zaidi za kisheria.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa abiria walitozwa nauli ya Sh. 800 badala ya Sh. 500 kwa safari ya ruti hiyo.
“Huo ni ukiukwaji wa Kanuni namba 34 na 35 ya Kanuni za Leseni ya Usafirishaji kwa Magari ya Abiria ya mwaka 2007,”– Kisaka.
Aidha, wamiliki walitakiwa kuwasilisha barua zenye maelezo na vielelezo kuhusu hatua zilizochukua dhidi ya dereva na kondakta.