MVUA YAFURIKISHA MITARO MAENEO YA BAMAGA-MWENGE, DAR


Maji yakiwa yamejaa katika uelekeo wa kituo cha Sayansi kutokea Bamaga-Mwenge.
Basi likipita kwenye maji yaliyofurika.
Mkazi wa jiji akikatiza kwenye barabara iliyojaa maji eneo hilo.
Wananchi wakitafakari namna ya kuvuka maji yaliyotuama barabarani.
Baadhi ya maeneo na vibanda yakiwa yamezingirwa maji.
MVUA ya muda mfupi iliyonyesha jijini Dar es Salaam na maeneo ya jirani asubuhi ya leo iliyaacha maeneo mengi yakiwa yamejaa maji na kusababisha shida kubwa kwa wakazi wa jiji hili.  Baadhi ya maeneo yaliyokumbwa na kadhia hiyo ni Bamaga-Mwenge ambako mitaro yenye kusafirisha maji ilijaa na maji kufurika hadi katika barabara na kufanya magari na waenda kwa miguu kupata shida.
(Na Gabriel Ng’osha/GPL)

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini