NDEGE YA FASTJET YASHINDWA KUTUA JIJINI MBEYA

Ndege ya kampuni ya Fastjet imeshindwa kutua Mkoani Mbeya na kulazimika kurejea Jijini Dar es salaam kutokana na kuchafuka kwa hali ya hewa kulikoambatana na ukungu.
Ndege hiyo ilipaswa kutua saa 2 asubuhi katika uwanja wa ndege wa Songwe na kushindwa kutua na kulazimika kuzunguka hewani zaidi ya mara nbili ikitafuta mwelekeo.
Hali hiyo ilisababisha taharuki miongoni mwa abiria takribani 131 wakiwamo watoto kutokana na ndege kushindwa kutua.
Tuliogopa baada ya kuona imeanza kuzunguka zunguka hewani na tukaogopa kuwa huenda tukaanguka kwenye safu za milima ya Mbeya“alisema mmoja wa abiria.
Mratibu wa shughuli za ndege wa Shirika hilo Omary Idrisa alikiri hali ya hewa kuchagia ndege hiyo kushindwa kuruka.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini