Watu wawili wamefariki Dunia na wawili kujeruhiwa katika matukio mawili tofauti


Mawili tofauti ambapo katika tukio la kwanza maria hauule  mkazi wa Kijiji cha muhukuru songea vijijini mkoani ruvuma  ameuawa kwa kukatwa na shoka kichwani  na mume wake itwaye  salvatory ndimbo  na kasha mwili wake  kuutupa mto mkurumo.
Hayo yamesemwa na kamanda wa polisi wa mkoa wa ruvuma ACP Mihayo Msikhela Kamanda mihayo anasema chanzo cha  mauaji hayo ni ugomvi  wa kimapenzi ambapo marehemu maria haule mwenye miaka arobaini  alikuwa na uhusiano wa kimapenzi  na mwanaume mwingine aitwaye  anzekula na kutaka kuachana na  mumewe  salvatory ndimbo mwenye miaka sitini.
 
Jeshi la polisi linaendelea kumsaka mume wa  marehemu maria Bw. Ndimbo mbaye ametoroka baada ya kufanya unyama huo.
 
Katika tukio jingine kamanda mihayo amesema kuwa mwendesha bodabodan aitwaye haridi alifa amefariki dunia na watu wawili kujeruhiwa baada ya kugongwa na gari  yenye namba T934BTE,Toyota Mark TU lililokuwa likiendeshwa na mweka hazina wa CCM mkoa wa ruvuma Bw. Silimu Mohamed mbaye anashikiliwa na polisi.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini