MWACHENI DIAMOND AITWE DIAMOND!

MWACHENI Diamond aitwe Diamond! Hiyo kauli pekee unayoweza kuisema kufuatia wakali wa muziki wa R&B kutoka Nigeria, Peter na Paul Okoye ‘P-Square’ kuukubali uwezo wa kimuziki wa bwa’mdogo kutoka Tandale, Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, mchapo hatua kwa hatua huu hapa.
Bwa’mdogo kutoka Tandale, Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa madansa wake ndani ya Lagos, Nigeria. NI LAGOS, NIGERIA
Wakali hao walionesha kumpigia saluti Diamond baada ya kukutana naye kwenye tamasha la utoaji wa Tuzo za Wanamichezo Bora Afrika lililofanyika Lagos, Nigeria, usiku wa kuamkia Januari 9, mwaka huu. 

Kwa mujibu wa chanzo kilichoambatana na Diamond nchini humo, saa chache kabla ya shoo kuanza, P-Square walimuibukia kwenye Hoteli ya Eko aliyofikia jijini humo na kummwagia pongezi nyingi sambamba na kumshauri baadhi ya vitu vya kimaendeleo

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini